Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,161
- 1,493
Ni wajibu wa viongozi kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa ili kuwaletea maendeleo Watanzania, pale inapotokea Viongozi hawa wamefanya jambo nzuri ambalo yawezekana sehemu nyingine hawajafanya kwa kiwango hicho na wangeweza kufanya, basi ni muhimu viongozi hawa waliofanya vizuri tukawatia moyo na kuwapongeza kwa kazi nzuri waliofanya.
Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa kwa muda wa mwaka mmoja na miezi mitano kupitia mapato yao ya ndani wanayokusanya wameweza kujenga jumla ya vyumba vya madarasa 78 kwa Shule za Msingi na Sekondari, Matundu ya vyoo 199 kwa Shule za Msingi na Sekondari, nyumba za Walimu 14 pamoja na madawati 3302.
Miradi hii ni kwa sekta ya Elimu tu, ipo miradi mingine wametekeleza kama ya Afya , Kilimo, Barabara etc. Pia idadi hii ni nje ya vyumba vya madarasa Elfu nane (8000) vilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha hakuna Mtoto mwenye sifa za kwenda shule anayekosa kwenda shule wala kukaa chiini kwa sababu ya upungufu wa vyumba vya madarasa
Hongera na pongezi saana kwenu uongozi wa Halmashauri ya Rufiji, kuanzia Mbunge wa Rufiji, Baraza la Madiwani, Menejimenti (Mkurugenzi wa Halmashauri na timu yake ya CMT), Watumishi wote wa Halmashauri kwa namna ambavyo mmeweza kufanikisha hayo kwa kuweza kubana matumizi ya kawaida na Fedha zinazokusanywa kuelekezwa kwenye Miradi ya Maendeleo.
Hongera pia uongozi wa Wilaya ya Rufiji kuanzia Mkuu wa Wilaya na timu yake yote kwa kusimamia vizuri utekelezaji huu wa miradi, watoto wetu wote wanasoma kwenye vyumba vya madarasa vyenye madawati ya kutosha.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
View attachment 2479910
View attachment 2479920View attachment 2479921View attachment 2479924