Hongera Traffic Police Dar. Kasi hii iendelee 2016

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
812
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Kuanzia siku ya Jmatatu Tarehe 4, Jan 2015 nimeona mabadiliko makubwa katika njia ninayopita mara kwa mara kwenda na kurudi kazini (Posta-Mwenge-Tegeta).

Kipindi cha Rush Hours zote (Asb na Jioni) magari yanavutwa kweli kweli kwenda yanakoelekea, hii inatia moyo sana.

Nawapongeza sana kwa ari hii mpya ya 2016. Inaonyesha jinsi mlivyojipanga, kuanzia viongozi mpaka askari wa kawaida. Endelezeni kasi hii hii bila kupunguza, mnatusaidia kupunguza muda wa kukaa barabarani.

Watumiaji wa Bara bara nyingine tunaomba mtujuze km kuna mabadiliko.
 
Kwa mara ya kwanza leo nimeona traffic kakataa rushwa, maeneo ya kigamboni kule . Lakini alimwambia dereva apeleke abiria arudi, labda alichukua wakati hatupo.
 
Wawape na nguo kutoka na miili yao wengine tangu watoke depo hawajepewa mpya na washanenepa unakuta nguo zimewakamata
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Kuanzia siku ya Jmatatu Tarehe 4, Jan 2015 nimeona mabadiliko makubwa katika njia ninayopita mara kwa mara kwenda na kurudi kazini (Posta-Mwenge-Tegeta).

Kipindi cha Rush Hours zote (Asb na Jioni) magari yanavutwa kweli kweli kwenda yanakoelekea, hii inatia moyo sana.

Nawapongeza sana kwa ari hii mpya ya 2016. Inaonyesha jinsi mlivyojipanga, kuanzia viongozi mpaka askari wa kawaida. Endelezeni kasi hii hii bila kupunguza, mnatusaidia kupunguza muda wa kukaa barabarani.

Watumiaji wa Bara bara nyingine tunaomba mtujuze km kuna mabadiliko.
Inaelekea wewe ni mgeni Wa hili jiji la DSM, kwa taarifa yako kwa msimu huu hilo unaloliona ni jambo la kawaida kila mwaka, kipindi hiki ambacho wafanyakazi wa mashirika na ofisi nyingi wanakuwa mapumzikoni, na wanafunzi kufunga shule foleni huwa inapungua sana. Itakapofika katikati na kuelekea mwisho Wa January, mambo yanarudi kama kawaida. Nakushauri ufuatilie hili utajifunza kitu
 
Ndugu hiki ni kipindi Cha likizo hali uionayo ni ya kawaida sana kwa DAR na majiji mengine mengi humu duniani. Subiri shule zifunguliwe kisha uje utupe mrejesho wa foleni!!
 
Kwa hiyo ruti uliyousema nachelea kukuunga mkono kwa sababu tajwa hapo juu..watumishi,wafanyakazi na wanafunzi wengi hawajarudi barabarani bado,tuangalie mpk katikati ya Jan to Feb japo ni kweli hawa jamaa wanajitahidi sana kuvuta magari..yaani wakiita wameita hata dk5 mnanyoosha tuu.
 
kumbuka mnavyoitwa upande mmoja dakika 5 upande mwingine unachelewa pia.
 
Ndo maana tunasema 'Rush hour' kama askari usalama barabarani wanajua flow ya magari kwa muda husika ni kutoka wapi na kwenda wapi..upande wenye magari mengi lazima uangaliwe.Kumbuka utaratibu wa asubuhi lane 2 zinaenda lk jioni lane 2 zinarudi kwenye barabara ya lane 3!!!
 
Inaelekea wewe ni mgeni Wa hili jiji la DSM, kwa taarifa yako kwa msimu huu hilo unaloliona ni jambo la kawaida kila mwaka, kipindi hiki ambacho wafanyakazi wa mashirika na ofisi nyingi wanakuwa mapumzikoni, na wanafunzi kufunga shule foleni huwa inapungua sana. Itakapofika katikati na kuelekea mwisho Wa January, mambo yanarudi kama kawaida. Nakushauri ufuatilie hili utajifunza kitu

Siyo kwamba ni mgeni, lah. Ndio maana nimeongelea kuanzia J.3 ya wiki hii wala sijaongelea Dec ambapo wengi walikuwa bado likizo. Kuanzia j.3 magari yalikuwa mengi sana lakini namna walivyohandle ni poa sana.
 
uchunguzi wako batili,,subiria muda tajwa hapo juu mambo yaleyale ,,halafu pale stanbic wanatubaniaga sana watu wa main road,,utakuta wanaita kindondon hata dk 10 lakini main road dk 5 hazifiki,,wanarudi masaki,,yaani pale ni kichefuchedu sijui unatembeaga mgao
 
Back
Top Bottom