Hongera! Tanzania SAFARI Chanel....

No Escape

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
6,663
7,738
Naanza kwa kusema HATUJACHELEWAA,Mara chache sana nchi kukupa siri ya mafanikio yake mpaka kufikia hatua ya maendeleo iliyofikia.
Imani yangu mimi naamini sekta ya UTALII inazitoa nchi nyingi sana duniani hasa UTALII WA NDANI".Katika miji niliyotembelea duniani UTALII WA NDANI upo juu kuliko huu wa kutegemea watalii wa nje,Bado mpaka leo sijaamini wazungu wanatuzidi nini sisi ndio wenye vivutio vingi vya Asili ukienda huko kwao utakuta wametengeneza MILIMA,WANYAMA MABWAWA MPAKA MITO...Hivyo vitu walivyotengeneza wanavipambapamba hatari kwa nini sisi Hatuwezi wakati tunavyo vya Asili.

>Ushauri wangu Chanel Hii itumike ipasavyo kukuza utalii wa ndani na iwekwe kisasa zaidi kutokana na maendeleo ya teknolojia Tutaona faida yake muda si mrefu pia inahitaji ubunifu wa hali ya Juu!!
1547710871020.png
1547710871020.png
 
Kila saa video ndio zile zile za wa handzabe zinachezwa masaa 24. Kipindi cha jana ni sawa sawa na cha juzi na cha kesho
 
Tangu Uzinduzi Hadi Sasa Hivi Picture Zile Zile
Hivi Utaangalia Nini Humo Ama Ndiyo Uzalendo
Picture Nyingi wanazoonyesha Tayari TBC Tumeziona Muda Sana
 
Tutafika tuu mwanzo mgumu....Mi ntaendelea kuangalia tuu kwa sababu sijawahi kuyaona haya!
 
ni hatua nzuri sana hii kwa serikali ya jJPM, hili suala lisiishie hapo liende mbali zaidi hadi kuonesha matarajio ya Tanzania kwenye sekta ya utalii kwa miaka 50 ijayo.

Ingekuwa vizuri kama serikali kupitia wizara ya utalii ingeandaa DVD/CD nzuri na zenye viwango vya juu zenye kila kila kitu kinachohusu utalii wa Tanzania halafu kila balozi anapewa hiyo CD na balozi anatoa kopi nyingi , anaitisha kikao na watanzania waishio nje na kuwatangazia juu ya adhma hiyo ya serikali.

kila mtanzania aishiye nje atakapopata CD aweze kuwashawishi watu kuitazama, ninajua wengi watashawishika kirahisi ila itakuwa ngumu.
 
Naanza kwa kusema HATUJACHELEWAA,Mara chache sana nchi kukupa siri ya mafanikio yake mpaka kufikia hatua ya maendeleo iliyofikia.
Imani yangu mimi naamini sekta ya UTALII inazitoa nchi nyingi sana duniani hasa UTALII WA NDANI".Katika miji niliyotembelea duniani UTALII WA NDANI upo juu kuliko huu wa kutegemea watalii wa nje,Bado mpaka leo sijaamini wazungu wanatuzidi nini sisi ndio wenye vivutio vingi vya Asili ukienda huko kwao utakuta wametengeneza MILIMA,WANYAMA MABWAWA MPAKA MITO...Hivyo vitu walivyotengeneza wanavipambapamba hatari kwa nini sisi Hatuwezi wakati tunavyo vya Asili.
>Ushauri wangu Chanel Hii itumike ipasavyo kukuza utalii wa ndani na iwekwe kisasa zaidi kutokana na maendeleo ya teknolojia Tutaona faida yake muda si mrefu pia inahitaji ubunifu wa hali ya Juu!!
View attachment 996968View attachment 996968
Utalii si wanyama tu, wasijikite sana kwenye vivutio vinavyojulikana vipo vingi sana hasa nyanda za huu kusini na pia wawashirikishe wanavijiji kwani baadhi ya vitu vipo lakini vimesahaulika.
 
Back
Top Bottom