Hongera SMZ kwa mataa barabarani

bartenderznz

JF-Expert Member
Jul 18, 2016
398
195
Imenifuruisha, si kwa kiwango kikubwa kwa kuwa nahisi huu mradi bado unaendelea, nitafurahi zaidi pale mji mzima kwa maana barabara zote kubwa ziking'aa usiku kucha.
 

Attachments

  • 1469177232280.jpg
    1469177232280.jpg
    53.2 KB · Views: 26
Mkuu mradi huu ni nchi nzima. Tueke pembeni ushabiki wa kisiasa Dokta Shein kafanya mambo makubwa katika kipindi hichi wapinzani walichomsusia kuliko Raisi yoyote alietangulia baada ya Karume wa kwanza.
1. Mradi mkubwa wa maji safi na salama ambapo mabomba ya maji yamesambazwa nchi nzima kitu ambacho kilionekana hakiwezekani.
2. Mradi mkubwa wa mitaro ya maji ya mvua ambapo suala la maji kutuama katika makazi ya watu litakua historia.
3. Ujenzi wa majengo ya kisasa ya ya ofisi za serekali. Skyscrapers.
4. Ukarabati mkubwa wa majengo ya kihistoria yanayopendezesha mji.
5. Ujenzi wa shule za kisasa kama ulaya zikiwa na fenicha kamili nchi nzima. Hakuna tena kukaa chini.
6.ujenzi wa nyumba za kisasa za makazi ya wananchi.
7. Ujenzi wa maduka ya kisasa yaani shopping Malls.

Hongera dokta shein.

Ombi moja kwako mheshimiwa waachilie huru mashehe wa uamsho wakajumuike na familia zako naamini hawatoleta tena chokochoko za kuhatarisha usalama wa nchi.
 
Back
Top Bottom