Hongera sana RC Magesa Mulongo - Arusha yenye neema kupitia wewe inawezekana.

Joseph Peter

Member
Oct 18, 2011
40
39
Kweli wajinga ndo waliwao, Lema na chama chake hawahudhurii vikao vya madiwani manispaa ya arusha zaidi ya kuchukua posho tu. Kazi ya kutetea rasilimali za manispaa ya arusha inafanywa kwa uzalendo mkubwa na Mkuu wa Mkoa Magesa Mulongo Mpiganaji wa kweli wa vita ya wanyonge.

Alikwenda manispaa kukagua miradi ya maendeleo na kuwaambia kuwa kuna harufu ya ufisadi hivyo atawapelekea tume ili haki itendeke na ionekane kuwa imetendeka. Na kweli kapeleka tume ya watu wa PPRA.

Tume hiyo itaangalia mambo yafuatayo:
1. Mradi wa Bank ya Dunia
2. Ujenzi wa choo cha soko la sanawari kwa zaidi ya 40 Millioni
3. Ukarabati wa round about ya kijenge kwa zaidi ya 44 Millioni
4. Mradi wa ADB kwa zaidi 180 Millioni ambayo ni asilimia 30 tu.
5. Matumizi ya mafuta
6. Mchakato wa utoaji masurufu

Hongera sana Magesa Mulongo kijana mwenzetu, mshauri Lema nae aache utoto na aje muijenge Arusha.
 
Ameletwa arusha kufanya kazi ya siasa! hata ukaguzi wa manispaa yetu ameufanya kisiasa. sisi tunamjua huyo ni houseboy from bagamoyo!
 
Anajipendekeza kwa watu wa Arusha ili wasimpige tena nyanya apitapo sokini. Mageza aache unifiki tunachotaka sisi amalize kwanza kutatua mkokoro wa cdm na ccm kuhusu mambo ya ummea wa Arusha. Ndipo tutakapomwelewa!!!
 
huyu jamaa anaelekea ni mchapa kazi aliyeletwa kazi maalum,sasa sijajua hiyo kazi maalum ni ipi.
 
Tume hiyo itaangalia mambo yafuatayo:
1. Mradi wa Bank ya Dunia
2. Ujenzi wa choo cha soko la sanawari kwa zaidi ya 40 Millioni
3. Ukarabati wa round about ya kijenge kwa zaidi ya 44 Millioni
4. Mradi wa ADB kwa zaidi 180 Millioni ambayo ni asilimia 30 tu.
5. Matumizi ya mafuta
6. Mchakato wa utoaji masurufu


Auditors wa Manispaa wanaafanya nini kama Tume inaletwa kwa gharama kubwa kufanya mahesabu ya choo cha sanawari??
Na kama RC amefanya kazi ya kuleta tume well, je matangazo mengi ya nini?
 
Back
Top Bottom