kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,872
Juzi jumatano nilitoa mada hapa wenye kichwa USHAURI KWA MABINTI ikiwa na dhumuni la kuwaasa dada zetu kuwa na kauli nzuri kwa wanaume hasa pale wanapotongozwa na wanaume hao.
Niliwashauri kuepuka kutukana wanaume pindi wanapowatokea badala yake wakatae kwa lugha nzuri tena iliyo laini. Wadada wengi walidhani natoa ya moyoni baada ya kutukanwa au kutoswa, nayaheshimu mawazo yao ila mimi tayari nina mke na nina furaha na ndoa yangu changa. Lakini hata kama ni kweli ingelikuwa nimetoswa hainizuii kukupa ushauri maana haya yamewatesa wengi na bado wanateseka na wangependa wapate namna ya kuyarekebisha ila is too late.
Back to the topic nadhani wengi wenu humu mlipata audio iliyotumwa na rapa Sterio akielezea namna anavyompenda rapa mwenzake binti anayeitwa chemical. Sterio alitoa ya moyoni kupitia EA Radio na kuelezea mengi sana juu ya feelings zake kwa chemical.
Baada ya hapo Dullah wa EA Radio akamtafuta chemical na kufanya naye interview kutaka kujua maoni yake juu ya alichokisema Sterio. Kwakweli huyu binti japo ni mdogo ki umri pamoja na usanii wake alijibu maswali aliyokuwa anaulizwa ki utu uzima sana, alijibu kama binti anayejielewa tena kwa ustaarabu mkubwa kwa STERIO mwenyewe na wasikilizaji, kama ulimsikia akihojiwa nadhani unaweza kuelewa hiki ninachokisema ila kama hukusikia unaweza tu kuingia google hapo utafute mahojiano hayo kisha ujifunze kitu kwa huyu binti.
Nazidi kuwaomba dada zetu mjifunze kwa watu kama hawa maana kwa mabinti wengine maarufu au hata wasio maarufu wangemshushua sana jamaa, wangesema mengi kutafuta kiki au hata kumdhalilisha huyu kijana.
Narudia tena wadada mjifunze kuwa na uvumilivu kwa majibu yenu kwa wanaume, najua tunakera sana, najua sisi ni ving'ang,anizi sana, najua hatusikii sawa lakini lugha nzuri ni jambo la msingi maana hata huyo msumbufu ukimjibu vzr tu kwa nidhamu anakuelewa ila ukijifanya wewe ni mzuri zaidi ,unajua kutukana zaidi siku zinakuja utabadili makanisa ukitafuta mume.