masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,172
Wiki iliyopita Mh Dr John Pombe Mgufuli, Waziri wa Ujenzi, akiongea na Makandarasi wa Kitanzania, alipngea kitu ambacho mimi binafsi kimenifurahisha sana.
Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB(Contractors Registration Board), ilifanya kikao cha majadiliano na makandarasi nchini.
Mh Dr Magufuli alialikwa kufunga mkutano huo na kutoa nasaha zake.
Ndipo Magufuli akasema wazi kuwa sekta ya ujenzi nchi karibu zote duniani huwa inamilikiwa na wajenzi wazalendo.
Magufuli alisema Mantiki ya sekta kumilikiwa na wazalendo ni mkakati wa kuhakikisha fedha yetu inabaki nchini.
Magufuli alibainisha kuwa yeye na serikali watahakikisha wazalendo watapewa kazi ili kufanikisha azma hiyo.
Hapo nampa big up Mh Magufuli na Dr JK kwa uamuzi huo maana ni uamuzi mgumu na umepigwa vita na watendaji kwa miaka mingi.
Nikiwa kama mjasiria mali nampongeza sana Dr Magufuli kwa uamuzi huo wa makusudi maana najua jinsi watendaji wabinafsi wanavyopindisha sheria ili kuwanyima wakandarasi wazalendo kazi za ujenzi.
Mfano hai wa hivi karibuni ni aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Ephraim Mrema na kazi alizotoa kwa wingi kwa wachina wake.
Kwa kutambua umuhimu wa uzalendo hongera sana Mh Magufuli.
MODS nimeiweka tena mada hii kama mada inayojitegemea ingawa mliiunganisha na majibu ya Mh Magufuli Bungeni, vitu ambavyo ni vitu viwili tofauti na havihusiani.
Tumpe moyo Mh Magufuli na viongozi wengine wanaoonyesha uzalendo kwa KUWAPENDELEA watanzania katika kuwapa miradi ili kukwa mua uchumi wetu na kubakisha fedha zetu nchini humuhumu.
Jana nimemsikia hata Mzee Mengi akitetea jambo hilohilo la uzalendo wa viongozi wetu kuwaweka WATANZANIA KWANZA katika kutoa kipaumbele cha kuendeleza rasilmali zetu nchini na tenda za kazi.
Katika nchi hii watanzania ndio first class citizens, na ndio jambo linaloongelewa hapa, na si vinginevyo.