Hongera sana Maxence Melo

Sijui ni lini utaamua kwa dhati kumwaga mchele kwenye kuku wengi wafaidike Kamarada.
Hapana Kamarada Mimi ni sawa tu na punje ya Chumvi ndani ya Maji ya Bahari ya Hindi.

Katika wale Wanyonge ( Masikini ) wa Kutukuka tuliokuwa tukiimbwa na Hayati nami ni Mmoja wao.

Hata Mimi ni kama Wewe tu niwapo hspa Jamvini ambapo huwa tunafaidika vyema na Wajuvi.
 
Hongera na pongezi zimuendee mkuu Maxence Melo kwa dhati kabisa kuanzisha Forum hii aisee
Sijui nisemaje ili nieleweke
Tangu niijue Jamiiforums nilipata experience kubwa Sana kuliko miaka niliyokaa darasani nikiwa mtupu na mweupe kichwani,

Nimeelimika na kupata exposure humu na leo najivunia maarifa niliyovuna humu pia nawapongeza members wote kwa kutoa michango hasi na chanya iliyonijenga katika nyanja zote kiujumla,

Bila kusahau jitihada zenu za dhati kuijenga forum hii kwa miaka yote bila kukata tamaa na kurudishwa nyuma na yeyote,

Kiufupi nishakua addicted na hii forum ikipita nusu saa sijalog in akili yangu hua inaanza kudemka,
JF imekua sehemu ya maisha yangu daima.

Ishi Sana mkuu Max

Nawakubali Sana wadau wote humu

Nishamaliza kudemka hivyo ndukiiiiiii!🏃🏃🏃
 
Kwa heshima na taadhima, nakupongeza na kukushukuru sana Maxence Melo kwa kubuni jamvi hili zuri na kulisimamia vema tangu ulipolianzisha miaka mingi iliyopita.

Nakuvulia kofia, Mkuu. Mimi binafsi nimepata faida nyingi sana humu. Kupitia jamvi hili nimeelimika kisiasa, kiafya, kibiashara na hata kiroho. Nimepata habari za kitaifa na kimataifa kwa wakati mwafaka. Na pia nimeongeza ujuzi wa lugha ya Kiswahili kupitia jamvi hili.

Kwangu mimi JamiiForums ni zaidi ya Redio na TV. Ndiyo sababu nimeona vema leo niseme asante sana Mkuu pamoja na timu yako (inayofanya kazi bila kuchoka kuhakikisha vigezo na masharti ya uandishi wa nyuzi, vinazingatiwa). Hata Maandiko Matakatifu yanatuambia "mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, tuyatafakari hayo." (Flp 4:8).

Mwisho, ingawa sio kwa umuhimu, nawashukuru Waandishi na Wachangiaji wa nyuzi mbalimbali. Mnaifanya JamiiForums izidi kung'ara. Mungu awabariki sana wote.
Mataga hawaipendi JF, watakuambia ni ya Chadema.
Wanasahau ukosoaji mkubwa wanaouona humu ndiyo mawazo na mtazamo wa watanzania juu ya watawala wa ccm.
 
Maxence Mubyazi Melo anastahili heshima iliyotukuka kutoka kwetu sisi wengine tuliokesha nae miaka yote ya Jiwe bila kuteteleka na kuwa hai Mpaka hivi leo, tunamshukuru sana kwa professiolism yake!! Ama sivyo kwa jinsi tulivyokuwa tunawindwa, he could have easily sold us for thirty pieces of silver BUT he resisted to the end inspite of all the hardships he had to endure! Bravo Mubyazi.
Kama JF imeweza ku survive mpaka dakika hii pamoja na vita yote ya mwendazake basi ninaweza kukiri kwamba JF will last forever na watu watapita waiache....
 
Baada ya Kumaliza Kidato cha Sita sikuona tena haja ya kwenda Chuo Kikuu kupata sijui Degrees, Masters na Doctorates ambazo wengi wenu ( siyo Wote ) mnazikimbilia na bado haziwasaidii na hazijawasaidia kwa lolote lile lenye Tija Kwenu Binafsi na kwa nchi yetu hii ya Tanzania

Kujiunga Kwangu tu hapa JamiiForums na Maarifa makubwa niyapatayo, kuimarika Kwangu kwa Kujenga na Kukabili Changamoto za Kitaaluma na Kifikra najiona si tu nina Degree bali sasa nina PhD yangu kutoka JamiiForums University.

JamiiForums imeimarisha sana uwezo wangu wa Kufikiri na ndiyo maana mara kwa mara nimewahi kusema kuwa ifike mahala sasa ama Serikali imtambue Mtani wangu wa Kihaya Maxence Melo kwa kumpa Tuzo ya Juu ya Heshima au basi Sisi Members wa JamiiForums tumfanyie Jambo jema na la Kutukuka kabisa kwa Ubunifu wake huu ambao una Tija kubwa kwa Ustawi na Maendeleo ya Taifa la Tanzania na Sisi Watanzania pia.

Naamini Serikali ya sasa ya Rais Mstaarabu na Muungwana asiye na Chuki ( Kisununu ) wala Kisasi, Ubabe na Ukatili ( Roho Mbaya ) Mama Samia Suluhu Hassan ( ambaye bahati nzuri nae ni Mwenzetu hapa na huwa tunakesha nae 24/7 ) ataliona hili na Kumtunuku huyu ' IT Guru ' Maxence Melo na Kampuni yake nzima bila kuwasahau na Wafanyakazi ( Watendaji ) wake wote kwa Kazi kubwa, ngumu na sometimes ya Hatari wanayoifanya.

Hii aifanye tu independent entity serikalin..akae nao awape uwezo..kwangu hiikama TISS tu. Hiki ni chuo kikuu.. niungane na ww kuhusu jina zuri Jamii forums university.

Kutokana na nchi hii kutokuwa utaratibu wa kujisomea, summary za nyuzi wanazopost wadau.zinanifanya nipate mambo mengi mapya
 
@Mexence Melo, ni mwamba, yaaan igneous rock, kwaan kupitia Jamiiforums watu twaeza tema nyongo kwa uhuru sana.

Hakika ww ni mzalendo, unawapenda na kuwapa thamani watu,

Ulifaa kuwa raisi wa nchi hii baada ya kifo cha magu na siyo huu utopolo wa 666sir 100 kigogo2014

Waitu nibakasinge, otaliwao, omkama akubele

Appreciation to you Maxence Melo
 
Back
Top Bottom