Hongera sana Elizabeth Michael "Lulu"

Tangu afariki Marehemu Kanumba industry ya filamu imeshuka Sana lakini Leo hii nimebahatika kuona filamu ya Lulu Michael au Elizabeth Michael kupitia YouTube. Movie hiyo inaitwa "Ni noma" Ni kazi nzuri Sana Cha kwanza nilichopenda hakukuwa na ile tabia ya msanii mmoja kuwa kwenye maeneo mengi unakuta producer yeye, director yeye n.k ndio maana kazi imesaidia kuwa nzuri.

Jambo la pili lililo nivutia ni maudhui ya filamu kiujumla amejitahidi kwenda kwenye idea tofauti na movie nyingi za bongo movie maudhui inamuhusu mwanamke ambaye anaishi maisha ya ukanjanja ana foji veti ili apate kazi ikiwa Hana elimu hiyo na mwanamke huyo amecheza Lulu je swali anawezaje kumudu kazi ikiwa Hana elimu hiyo?ukiicheki utapata jibu

Vitu vilivyonivutia ni usheshi ambao upo serious kwenye hii filamu pia quality ya video ipo vizuri.

Washiriki wote waliocheza hii filamu wameitendea haki kabisa, wamevaa vizuri uhusika ikiwemo dude, isarito n.k

NB: Ikiwa mtatoa kazi nzuri Kama hii itasaidia kupandisha soko lenu la filamu.

Nipoteze bando kuangalia bongo movie seriously???

Unanunua bando kabisaaa???

Kila la kheri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom