Hongera sana Clifford Mario Ndimbo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera sana Clifford Mario Ndimbo

Discussion in 'Sports' started by Jacobus, May 12, 2011.

 1. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,580
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Napenda kumpongeza Ndimbo kujiuzuru nafasi ya usemaji wa klabu ya Simba. Hata hivo uamuzi wake umechelewa kwani sie tuliona mapema hali hiyo ya kutofuata sheria na taratibu.
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  sheria na taratibu zipi zilikuwa hazifatwi..
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Rage anamdharau sana ndimbo,anasema yeye hashughulikii ajira ndogo ndogo za makarani,hapo hapo anajikanganya kuwa fifa walisema ofisa habari awe mwajiriwa wa kudumu!Ni ngumu kufanya kazi na rage
   
 4. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280
  Huyu naye Azam. Jamaa kapandiwa Dau na Azam, Mengine anayosema ni Formalities za most of resignations.
   
 5. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280
  Hii kauli ya huyu mzee na mimi imeniacha hoi. Ila ni mambo ya kawaida sana katika resignation issues
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Maha-Rage mwenyewe shule ndo matatizo,analewa sifa za uongozi.Karibu mtaani Ndimbo.
   
 7. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,141
  Likes Received: 3,330
  Trophy Points: 280
  i knew it!! jamaa aliacha kazi yake nzuri kama tv presenter pale tbc1.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  sasa nsjua kwa nini RAGE alifungwa. hope angeozea huko
   
 9. c

  chetuntu R I P

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ulikuwa mawazoni mwangu, jamaa ni mjuaji sana hata technical issues. Wapiga kura wake wana kazi.
   
 10. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Mm ni mwanachama wa simba hata mm nampa pongezi ndimbo anajua anachokifanya na muhimu ni kujitambua,big ndimbo maisha hayapo simba,wasidharau watu kwa vyeo vyao
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  dogo muoga sana huyu...vita ni vita muraaa...pigana mpka mwisho yaani kujiuzuru haisaidiii alipaswa kuwa na ngozi ngumu yenye kuhimili michubuko hiyo aliyofanya sio kabisa...Mi naona kafanya uamuzi wa kitoto na kuanza kulia lia kwenye vyombo vya habari...hakuweza ku demonstrate maturity katika kuhandle issues ndo maana wamemwita karani...
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  Msomali haachi asili yake
   
 13. R

  Rugishar Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: May 5, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kufanya kazi na Msomali siyo mchezo.
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Pesa za TP Mazembe zitaipeleka Simba Pabaya. yaani swala la mikwanja ya TP Mazembe Rage hataki mtu alete kiwingu, yaani hata kumpa mikaratasi mitupu msemaji wa klabu ili akawatangazie waandishi wa habari Huyu msomali hataki. halafu pili huyu Msomali anaitumia Simba kama Promo yake ya kisiasa, kwa hiyo anaona msemaji wa klabu ndio atakuwa anapata ujiko kuliko yeye. huyu alishafungwa jela kwa kesi ya wizi wa wazi kabisa sasa uaminifu huo kwa huyu Msomali sijui unatoka wapi!
   
 15. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sio kufungwa tu aliwahi kufukuzwa kazi CDA kwa wizi wa pesa,huyu jamaa kwenye fedha ni mtu wa kuogopwa kama mwenye ukoma
   
 16. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #16
  May 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ila ndimbo na yeye ni mtu wa jabu sana atajiuzulu vipi kabla ajaandika barua?Bado sijajua elimu ya ndimbo,maana nasikia ametuma e amil ya kujiuzulu na sio barua.Sasa hiyo mpya ya mtu kutuma e mail badala ya barua.Kazi ipo sana kwa uongozi wa Rage simba sijui?????????????
   
 17. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 1,262
  Trophy Points: 280
  ..ndimbo yuko sahihi..nilijua anajiuzulu siku tatu kabla.....msemaji wa club anatuma email kwenye intenet cafe....hana ht laptop....pia Rage boya wa mambo..waswahili husema kujua kwingi mbele kiza...kama mnakumbuka aliwahi kusema amekatia rufaa Caf timu ya Tp Mazembe na ana uhakika atashinda mpk leo kimya..jamaa wanacheza makundi sasa CAF..juzi karopoka eti yanga wanajihangaisha kwa Asamoah mwisho wa siku Asamoah yuko Jagwani..
   
 18. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #18
  May 16, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,580
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Nawashukuru sana kwa kuliona tatizo la Rage, lakini ni sahihi kumlaumu yeye binafsi?
  Mie nipo tofauti kidogo na naona wa kulaumu ni wale wanaompa kila akitakacho:-
  1. Wakazi wa Tabora= pale ana vyeo vingi mno kana kwamba hawaoni hakuna mwingine ila yeye kama ni muarobaini.
  2. Wanachama wa Simba= katiba ya klabu ilikiukwa kwani rage ni mkaaji wa Tabora, sasa ni mbunge.
  3. TFF= kumruhusu kuingia uwanja wetu wa taifa na jamaa zake wa klabu ndogo ya England eti kuukagua. Haya ni matusi kwetu watanzania, uwanja huu si wa klabu yoyote ni wa wananchi mbona FIFA/CAF na hata CECAFA wameuidhinisha kwa mashindano yao mengi tu kufanyika hapo hata timu bora kabisa kwa soka ya taifa linaloheshimika la Brasil imecheza hapo sasa haiingii akilini leo watu wajifanye wanaukagua, je wangesema haufai ingekuwaje?
  4. Waandishi wa habari= Wanampa nafasi mno ya kujinadi.
  WATAFAKARI.
   
 19. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #19
  May 17, 2011
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,283
  Trophy Points: 280
  Mbona Rage mwenyewe ana vyeo zaidi ya vitatu tena vikubwa na bado ni Mwenyekiti wa Simba
   
Loading...