MANILABHONA
JF-Expert Member
- Apr 1, 2015
- 462
- 351
Nikiwa ni zao la ujauzito wa shuleni, mzazi wangu akapata nafasi ya kujiendeleza na leo kanifikisha hatua niliyonayo sasa, ninadiriki kumpongeza Baba Askofu wa Kagera kwa kuondoa ukimya na kulizungumza tatizzo hili ambalo wengi wamelifumbia macho na masikio kwa woga tu wa kutofautiana mtazamo na Mergfool,wengine wanaogopa kufungwa wengine kuwekwa kizuizini na wengine wanampaka mergfool mafuta kwa mgongo wa chupa-hawamwelezi ukweli, ni wanafiki hawampi taarifa sahihi kuhussu maoni ya wananchi.Ukweli ni kwamba tunatengeneza kizazi cha wajinga wasioenda shule, kizazi cha maskini, kizazi kitakachokuwa na afya duni. najaribu kuwaza kwa sauti baada ya miaka tuseme 10 tutakuwa tumetengeneza kizazi cha namna gani.Huu ni mzunguko wa kifo (shule hakuna --elimu hakuna--afya hakuna--umaskini--shule hakuna--elimu hakuna n.k). Hivi viongozi mliopo sasa kwa kila kosa mlilotenda kwa miaka 10 iliyopita lingezaa mimba mngekuwa wapi leo na watoto wenu hao wakakosa elimu- tafakarini kwa kina kabla ya kuamua
"Yeyote ambaye hajawahi kukosea awe wa kwanza kumpiga jiwe" na Yesu kristo alipoamka akakuta wote wameondoka. Akamwambia yule mwanamke amka enenda zako
"Yeyote ambaye hajawahi kukosea awe wa kwanza kumpiga jiwe" na Yesu kristo alipoamka akakuta wote wameondoka. Akamwambia yule mwanamke amka enenda zako