Hongera Salva Kiir - Rais wa Sudan Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Salva Kiir - Rais wa Sudan Kusini

Discussion in 'International Forum' started by Ileje, Mar 2, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Katika kipindi kifupi cha chini ya mwaka mmoja tangu nchi yako ipate uhuru tarehe 9/7/2011 juhudi zako za kuwaondolea umaskini wananchi wako tumeziona;
  1. Kukuza kilimo na kuondoa njaa kutokana na vita vya muda mrefu - HONGERA
  2. Elimu na kujenga uzalendo wa wananchi wako - HONGERA
  3. Kuzuia wizi wa mafuta uliokuwa unafanywa na Sudani Kaskazini - HONGERA
  4. Mradi wa ujenzi wa reli na bomba la mafuta kutoka Juba hadi Lamu Kenya - HONGERA
  Hivi Tanzania tunajifunza nini kutoka nchi hii changa?
  1. Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya - ZERO
  2. Mpango wa reli kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay (Mtwara Corridor) - ZERO
  3. Mabasi yaendayo kasi DSM - ZERO
  4. Kuimarisha reli ya kati kwa kuwa na treni zinazotumia umeme - ZERO
  5. Reli ya kutoka Tanga hadi Musoma - ZERO
  6. Kilimo kwanza - ZERO
  7. Elimu ya sekondari -ZERO
  8. Maji jijini DSM - ZERO
  9. Michezo - ZERO
  10. Usalama wa raia kutoka kwa polisi - ZERO
  11. Kuzuia rushwa - ZERO
  Wana JF wapi Tume ya MIpango! Wapi tunakokwenda!
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ... dah, nilidhani unamzungumzia Salva Rweyemamu kumbe ufanno tu wa majina!!
   
 3. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Si ni mafundi wa kusimamia ujenzi wa mabanda ya kuku, shule za chekechea na vitu vya namna hiyo ambapo wakati wa uzinduzi wake makamo wa rais ambaye anakuwa amelipwa hela nyingi za per dm yeye na wake zake pamoja na msafara wake wenye gharama mara 100 ya mradi anaouzindua!

  Utashangaa mradi wa ofisi ya kijiji anayozindua huyu makamu wa rais wa uzinduzi huwa haina hata thamani kulinganisha na gari aliyofika nayo hapo kwenye uzinduzi!
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Topic haifai hapa...
   
 5. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kwani wewe hukuona headline - kuwa ni Salva Kiir?!
   
 6. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hayo yote uliyoompa hongera mzee wa pama,,tunayathibitishaje?
   
 7. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Jana kwa mfano alikuwa Lamu Kenya ambako Rais Kibaki alikuwa anazindua ujenzi wa bandari kubwa ambayo itakuwa inatumika kusafirisha bidhaa kutoka Sudan Kusini kwa kutumia treni iendayo kasi na mafuta yatakayokuwa yanasafirishwa kwa bomba linalotarajiwa kujengwa.
   
 8. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kweli ni Aibu sana ila tutapambana tu hadi kieleweke...
   
 9. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wa Sudan wengi wapo Canada, Marekani na USA na walipelekwa huko na kikundi cha John Garang ambaye alisomea hapa Tanzania huko Tanga shule ya Magamba. NIna hakika wakirudi hao wataalam waliopelekwa nje kusomea fani mbali mbali ile nchi ina take off mapema na mabenki ya Kenya na makampuni yao yameshakimbilia Sudan.

  Sisi alienda Kikwete tu kwenye kuapishwa huyu bwana na sidhani kama alibeba na delegation ya kina Mengi 's na Bakhresa's kuwatambulisha huko.Hamna sehemu ambazo zina biashara nzuri kama ambazo zinazotoka kwenye machafuko. Uliza Mabenki na makampuni mengine yanavyopata faida huko Angola.
   
Loading...