Hongera Robert Gabriel Mugabe

Hongera Robert Gabriel Mugabe

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Kuapishwa kwako leo ni ujumbe tosha kwetu. Kwamba umri si lolote kwenye uongozi. 89 yako ni kuu.Kinachotakiwa ni uwezo,dira na mwongozo. Kila la kheri kaka Mugabe. Linda nchi yako. Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
...mmmh mkuu umri ni ishu bhana,piga average ya umri wa marais wa ulaya na marekani utapata kwenye 48. Ila wastani wa marais wetu ni 65. Tofauti ya kiutendaji wala huhitaji kamusi kuelewa...
 
Hongera zake Mr Mugabe,naupenda msimamo wako na kutowatetemekea US na UK...chapa kazi Babu.
 
Kuapishwa kwako leo ni ujumbe tosha kwetu. Kwamba umri si lolote kwenye uongozi. 89 yako ni kuu.Kinachotakiwa ni uwezo,dira na mwongozo. Kila la kheri kaka Mugabe. Linda nchi yako. Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Moja ya viongozi wachache waliobaki si Afrika pekee, bali dunia nzima, wanaoweza kusimama kidete kutetea maslahi mapana na muda mrefu ya nchi zao. Kwa Afrika nikiangalia kwa haraka simouni mwingine labda America ya Kusini wapo wachache japo Kamanda Hugo Chavez katangulia mbele ya haki. Baada ya miaka 20 au 30 ndiyo ukweli juu ya kifo chake utajulikana.
 
Hongera Mzee Mugabe, hata mimi namkubali. Ni kiongozi mwenye maono na anajua watu wake wanataka nini. Mugaabe hakuchaguliwa na wazazi wake, kaka zake na wala marafiki zake kwa maana wote ama wamekufa au ni wazee sana na waliosalia ni wachache mno. Hii inatuonyesha amechaguliwa na watu wneye umri sawa na watoto wake na wajukuu.

Wanauna msimamo wake na wamesoma historia ya nchi yao. Hawakuyumbishwa na msimamo wa nchi za magharibi. Hongera sana wazimbabwe, mmetuonyesha njia na kasumba ya umri ishindwe na ilegee.
 
Amenifurahisha sana leo kwenye speech yake alivyoweka msimamo kuhusu gays.
 
Umri miaka 89, madarakani miaka 35! I am proud I am not Zimbabwean ..
 
Back
Top Bottom