Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,204
- 3,277
Nimekukumbuka shujaa wa masikini Ulimboka, nakumbuka ulipiga kelele saaana wewe na madaktari wenzako ukiomba kuboreshwa kwa hospitali ya Muhimbilli, pia maslahi ya madaktari . Hakika baba uliteseka kwa ajili yetu wananchi wa maisha ya kati na masikini. Pamoja na hayo, baba uliambulia kupigwa kipigo cha mbwa mwizi na kung'olewa meno bila ganzi. Kibaya zaidi baba ukiwa na maumivu makali, ukatupwa kwenye msitu wa Mabwepande ukiawa nusu mfu, baridi, wadudu vyote vikawa juu yako baba huku ukichwagizwa na maumivu ya meno yaliyong'olewa bila ganzi.
Baada ya miaka mitatu Baba Rais Magufuli anakwenda Muhimbili na kushuhudia uozo aliokuwa ukiupigia kelele Ulimboka. Kitendo cha wewe baba kwenda Muhimbili na kuibua uozo, umeumbua Mashetani wa serikali iliyopita waliomng'oa meno Ulimboka. Sipependi kukulaumu Baba Magufuli, maana wewe wakati ule usingeweza kusema chochote maana ulikuwa chini ya Mfalme wa Msoga, ungesema kitu uenda hata leo usingekuwa Rais.
Namalizia kwa kusema, baba Ulimboka Watanzania wenye busara tukimuona Magufuli anaangaika na uozo wa Muhimbili, daima tunakukumbuka kwa damu yako iliyovuja kwa ajili ya Watanzania, daima utaendelea kuwa moyoni mwetu