Hongera Rais Magufuli kwa kufikisha siku 200 Ikulu

Ipililo

Senior Member
Dec 19, 2015
107
83
Mnamo 26, march 1983 Mzalendo Hayati Edward Moringe Sokoine alisema yafuatayo,

" Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta, kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra za Mungu na wananchi wake peke yake, VIONGOZI WAZEMBE NA WABADHIRIFU WAHESABU SIKU ZAO"

Ikiwa ni Siku mia mbili na ushee wa siku mbili tangu Amiri Jeshi Mkuu na Raisi wa Taifa letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh raisi DR MAGUFULI ameapishwa, ameonyesha kuishi na Kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2015 na yale yote aliyowaahidi watanzania pindi atakapopewa Ridhaa, Utendaji Utumishi,uwajibikaji,na Uzalendo wake katika kutekeleza majukumu yake kama kiongozi mkuu wa Nchi yetu ni DIRA kwa Watanzania waliopoteza matumaini kwa serekali yao .

kwa muda huo wa siku 200 tayari serekali ya Dr JPM imeonyesha uthubutu na umadhubuti wa kuyaendea na kuyasimami kwa ufanisi Mkubwa mambo makubwa na yamsingi kwa ustawi na maendeleo ya Taifa yapo mambo yaliokwamisha Ustawi wa Wa tanzania Kiuchumi na Kijamii kwa muda mrefu sana bila kupata majawabu lakini Dr JPM Amekuwa Mwarubaini wa Changamoto,kero na matatizo ya mtu mmoja mmoja, kikundi cha watu, jamii flani, taasisi serekali na Taifa kwa ujumla Ameweza kusimama imara na kuzisimamia mamlaka zilizo Chini yake ipasavyo.

HiiInanikubusha kule America wakati wa Raisi wa 32 wa Marekani( H.E) FRANKLIN D. ROOSEVELT (FDR) alipoingia Madarakani Alikuja na dhana Ya NEW DEAL huu Ulikuwa ni mpango mkakati wa kuivusha Taifa la Marekani Kutoka Katika changamoto mbalimbali Ndani ya siku 100 alikuja na dhana Ya NEW DEAL dhana ya Kuirejesha Taifa katika Mstari pamoja na kuhakikisha anamaliza changamoto za kitaifa na NEW DEAL Ilikuwa ni dhana inayobeba DIRA ya serekali katika kipindi cha mpito

Huu nimfano wa Dhana ya HAPA KAZI katika uongozi wa serekali ya awamu ya tano ya Dr JPM ambaye amewaza kupambana na mambo kaadhaa wakadhaa ikiwemo Kubana Matumizi ya Fedha za Umma Kurejesha Nidhamu Ya Kazi kwa watumishi,Kusimamia Makusanyo ya Kodi, Kupambana na Rushwa,Ufisadi,uzembe kazini,na kila chembe ya ubadhirifu ni kati ya siku 200 za DR JOHN POMBE MAGUFULI ikulu ndipo ambapo matabaka kati ya mwenye nacho na asiyenacho yanaondoka.

Ni ndani ya Siku200 za Dr JPM Ambapo uzembe katika utumishi na makazini umekwisha, ni ndani ya siku hizi 200 za Dr JOHN POMBE MAGUFULI ameweza kumaliza urasimu katika maeneo mbali mbali, hivi sasa uongozi ni dhamana, kiongozi yoyote anapopewa dhamana ya kuwatumikia au kuongoza eneo flani kwa niaba ya watanzania basi ajue amepewa wito wa jukumu la kitaifa na la kizalendo kwa maslai ya nchi na si maslahi binafsi kama ilivyo siku za nyuma.

Tumeona namna viongozi,watendaji na watumishi wa kaliba ya uvivu,uzembe,ubinafsi na urasimu walivyotumbuliwa mara moja ni ndani ya siku 200 MAGUFULI ameonekana kuwa Raisi mwenye Maamuzi thabiti na dhamira ya kweli kuivusha tanzania kuelekea Taifa Bora na lenye neema.

Ndani ya siku200 na Hapa Kazi Tumeona Dhima ya Uongozi ikirudi katika sifa za mwana tanu au awaku ya kwanza kwa sasa kuna utaofauti wa kimaadili kati ya kiongozi wa Serekali ya mh Dr MAGUFULI, na mfanya biashara ndani ya serekali Viongozi wametakiwa kutoshiriki mambo ya kibepari na ukabaila,wasiwe na hisa katika makampuni waliokuwa wakurugenzi katika makampuni ya kikabaila au kibepari wametakiwa kutofautiasha mambo hayo na kupunguza mishahara au kutokujilipa kama makabaila, kutokuwa na mishaara miwili au zaidi, Tunaona Ndani ya siku 200 Dr Magufuli Amefanikiwa kurejesha Miiko ya Uongozi Chini ya Azimio la Arusha

Katika wakati huu Taifa linapitia katika kipindi cha mpito tumeona namna ambavyo kumetokea mapambano kati ya wahaini walanguzi dhidi ya serekali,kumetokea kundi la wafanya biashara baadhi kutaka kukwamisha kwa makusudi dhamira ya Dr JPM katika kuliendesha Taifa ndani ya Awamu hii na katika mapambano hayo serekali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwakabili walanguzi wa sukari wenye lengo la kubujumu uchumi wa Tanzani hii ni ishara tosha ndani200 Raisi Ameonyesha kutosha Na Umadhubuti katika Mamlaka yake Hii inaonyesha Hakuna Tofauti Kati ya Dhana NEW DEAL ya Raisi wa 32 Wa Taifa la Marekani FRANKLIN D ROOSEVELT 1933 na HAPA KAZI ya Raisi awamu ya tano Dr JP MAGUFULI 2015 kwa kiasi kikubwa iwezo wa kiuongozi ndani ya siku 200 ni Instruments tosha kuonyesha dira ya serekali na wapi Raisi anakusudia Kuivusha Nchi.

Mungu Ibariki Africa, Mungu IbarikiTanzania.
 
Back
Top Bottom