Hongera nyingi kwa Jeshi la Polisi kukomesha mauaji Kibiti

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,970
2,184
Wakuu

Nitoe pongezi nyingi kwa jeshi letu la polisi likiongozwa na IGP Sirro kufanikisha kuyazima kabisa mauaji ya kutumia risasi yaliyoibukia huko Pwani kwa wilaya za mkuranga, kibiti na rufiji

Katika hili jeshi mmeonesha uadilifu mkubwa, Tanzania hususani Kibiti inarejea katika hali yake ya amani kama ilivyozoeleka hapo awali na shughuli za maendeleo zimejerejea pasi na shaka

Kamanda Sirro katika hili umefanikiwa!
Wananchi tuko pamoja na wewe hakika katika kuhakikisha uharifu unatokomezwa hapa nchini

Hongera saana jeshi la polisi Tanzania, Kibiti bila mauaji imewezekana



Mr Swax
 
We naona unataka kesho tuamke na bad news... Bora ukae kimya tu jamaa watulie. Huyo Sirro na vijana wake wanajua maadui wao ni wapinzani na wote wanaotambua na kutetea haki...

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
 
Sawa kabisa, pongezi kubwa kwa jeshi la polisi, wengi huwa tunajisihau hapa, sawa bado wana matatizo yao na raia kama ya kubambikiana makesi, rushwa na kujiona miungu mitu, ila taratibu wanajirekebisha, mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni..
 
Mauaji yanakomeshwaje?
Wauaji hawajauawa, kukamatwa wala kunyang'anywa Silaha?
 
Back
Top Bottom