kweli, nape ni kiongozi mahiri tena jasiri asiyeogopa mtu. mi hupenda kumwita nape the great.
bahati mbaya sana kijana huyu ana maadui wengi sana ambao wametia nia kutaka kumharibia hasa baada ya kuukwaa uwaziri. Kutwa kucha wanamvizia kumtoa makosa ili wawaaminishe watz kuwa kijana hafai na hakustahili kuwa waziri.
Makosa madogo madogo hata yale ya kimatamshi wanayashikia bango na kupiga kelele utadhani anga limedondoka.
Wanataka tuamini kuna dhoruba ndani ya kikombe cha chai. maadui hawa kamwe hawatamshinda nape, nape the great. nampongeza jpm kwa kumchagua nape kuwa waziri
bila shaka nape anafahamu kuwa ana maadui wengi, ndani ya ccm na nje (kambi yote ya upinzani).
Hii imetokana na kazi aliyokuwa akiifanya/anayoifanya ya katibu mwenezi wa ccm. kutokana na asili ya kazi yenyewe, ilibidi apambane na adui zake uso kwa uso, lakini aliwashinda.
Baada ya nyota ya nape kuendelea kung'aa, maadui zake wanamsagia meno.
namtahadharisha nape awe makini sana kiutendaji na kimatamshi kwani adui anasubiri uteleze akupige.
Baadhi wana silaha kali kuliko AK47. hao ni waandishi wa habari na kalamu zao. kuwa makini nao.
Rais amekuamini, usimwangushe.
go go go nape the great.