Hongera Mzee Lyatonga tumeona matunda ya kujipendekeza.

mndorwe

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
2,472
1,027
Hayawihayawi sasa yamekuwa ,kweli wewe ulisoma siasa zako bulgaria .Siasa hizi zimekupa manufaa. Umekuwa mwalimu wangu mzuri jana kwenye somo la kujipendekeza,hongera.
Kwanza nikupongeze kwa kukumbukwa na Rais na sasa wewe umeteuliwa kuwa mwenyekiti wa body ya parole nimeona faida ya kujipendekeza hongera.
Jana ulivyotoka jumuiya tu ndo ukapokea simu toka kule kitalani kuwa umeteuliwa niliona furaha yako usoni na mchoni hongera ,na wewe ulikubali tena kwa sauti kuu.
Ombi langu ni moja tu umepata ajira ya pili sasa kutoka hiyo ya bar hapa njiapanda na sasa hii ya kitaifa.Kwa mtini jifunzeni imeandikwa kwenye biblia ,mwenzako Mbatia kipindi kile alivyoteuliwa ulikuwa ukimdhalilisha sana kuwa mara ameteuliwa na Rais kwani yeye anavaa sketi ..ulihoji na kumpiga vijembe,ila Mbatia tutamkumbuka alivyoteuliwa alitujali sana ,wewe wajua alijitahid kujenga vyoo vya kisasa kwenye shule zetu,vyumba vya madarasa na hata mabwalo ya kuliachakula kwenye shule zetu.
Naomba mzee mrema ili baada ya miaka mitatu ukistafu tukukumbuke na ww ukirud rud na zawad mgongoni na sis tupate manufaa ya kujipendekeza kwako.
Kumbuka wale kina mama pale nje ya bar yako ,wanavyoteseka miaka yote umekuanao wakumbuke ,usiwasahau. Kumbuka malalamiko yao pale kuwa hakuna wateja wa kuwauzia nyanya ,viaz na ndizi hali ya uchumi ngum ukifika hapo kitalani kuapishwa mwambie rais kuwa hali ya kina mama imekuwa ngum.
Tutakukumbuka kama utafikisha kilio chetu maisha magumu,ili tupate faida ya kujipendekeza.
Naona pia afya yako itatengemaa kwani tangia Mbatia akuangushe 2015 umekuwa
wamawazo ,makubwa na huku watu wengi wa kikucheka, hongera sana.
Nimatumaini yangu utapita hapa kusoma hiki nilichoandika mzee ,si maneno mengi ila yachukue.
Hongera mzee mrema ukiwa hapa Kilaracha najua unajiandaa kwenda kula kiapo labda.Umetupatia sifa kuu wanavunjo na tumeona umuhimu wa kujipendekeza.
Ni mm kijana wako kutoka hapa Kilaracha, ila machinga kwa sasa Arusha...Hongera nimeona faida ya kujipendekeza.
 
Back
Top Bottom