Hongera ‘Mr President’, umetukosha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera ‘Mr President’, umetukosha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Sep 25, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  JUMATANO watu mimacho ikawa kwenye runinga zao, hata wale TBC ni chenga siku hiyo hawakuwa na shida maana TRENET ikawa live nayo hivyo hata wale ndugu zangu walokole wasioangalia vituo vingine nao wakawa wanafaidi.

  Watu wakajipanga kuuliza maswali, wengi wakashindwa kisa! Njia za simu zikawa hazipatikani, wengine wakaanza kuniandikia ujumbe kana kwamba mimi ndiye msaidizi wa Mr President! Unacheka nini? Ni kweli nilipokea sms tatu kiulaini kwa nini simu hazipatikani.

  Unataka niwataje majina ya waliolalamika? Aha ngoja niwaache maana watajisikia vibaya. Kidogo niwape namba ya Salva mzee wa mawasiliano pale Ikulu lakini bahati mbaya nikajikuta nakuwa busy kuandika alichotamka Mr President. Wakalalamika sms zao kutojibiwa na wengine kutoweza kupiga simu.

  Lakini wengine pia wakalalamika eti kwa nini maswali yao yanaanzia kwa mtu ndipo yaende kule studio ambako Rais alikuwa na mzee Tido!

  Sina majibu ila na mimi niwaambie tu kwamba swali langu pia halikujibiwa kwa hiyo washikaji tuko wengi ambao hatukujibiwa maswali. Lakini sio mmemsikia Mr President aliahidi kuwa atatujibu kupitia sms na mitandao yetu.

  Hata wasela wangu wa vijiweni kaeni mkao wa kula, si mmesikia Mr President anaweza kuvamia kijiwe chenu na kuruhusu mmuulize maswali kama mtakakuwa nayo, sasa washikaji nanyi someni basi magazeti angalau mwende na muda.

  Mnaonaje mfumo huu si utakuwa umezidi ule wa mzee Chavez wa Venezuela mwenye kutamba na kipindi chake cha Mr President.

  Wengi wamesifu mfumo huu kuwa unasaidia kuondoa kiu ya wananchi kuhusu masuala mbalimbali yanayowakera.

  Tuligubikwa kwenye waraka na ilani na miongozo ya kidini inayotuelekeza namna ya kupiga kura. Lakini maamuzi ya NEC nayo yakawa moto! Nadhani Mr President ameshayatolea ufafanuzi hivi kweli hapo kuna mtu atatia neno!

  Labda awe mchawi wa serikali yetu tukufu maana kama ni majibu mzee wa watu alijipinda kujibu kwa kirefu hadi mwingine akaniandikia mbona anajibu kwa kirefu vile.

  Sasa ulitaka ajibu kwa kifupi ili mbaki na dukuduku. Ndio maana mzee akaamua kutumia swali la walimu kujibu kwa zaidi ya dakika 15 wengine wakalalamika si dakika 90 atajibu maswali matano tu.

  Wengine wakadai walimu sio issue tena kwa leo, wengi wakataka maswali ya ufisadi, maamuzi ya NEC ya CCM na nyaraka za kidini za Pengo na wenzake bila kumsahau Sheikh Ponda wa shura ya maimamu.

  Ohoo! CCM inashabikia ufisadi, ohoo wabunge wamezibwa midomo? Mr President alifafanua kwamba wabunge jamani hamjazibwa midomo, endeleeni tu kuelimisha na kukosoa pale mnapoona mambo hayaendi.

  Mzee Ole Sendeka umeisikia hiyo? Kimaro hapo Vunjo upo? Dk. Mwakyembe endelea tu na wewe Mpendazoe usirudi nyuma lakini endelea kushirikiana na dada Beatrice.

  Lakini salamu hizi pia mfikishieni Selelii mzee wa kuwalaani mawaziri.

  http://www.habarileo.co.tz/safu/?n=3611
   
 2. G

  Genda Member

  #2
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Majuzi tulifurahia kumwona Rais "eti" akizungumza ana kwa ana na wananchi kupitia runinga ta TBC iliyounganishwa kwa simu za kila aina zilizopo nchini.

  Sentenso yangu iliyopita ina neno "eti" kwa makusudi ya kuamsha changamoto ya "vya usasa" na kusahau hali halisi yetu.

  Tanzania yetu inageuka kuwa ya teknolojia ya kisasa!

  Kwa nini isitangazwe tu kwamba Rais alizungumza na baadhi ya "wenyenazo" (the haves) na kuwasahau walalahoi wengi ambao hawana hata ndoto ya kumiliki "sms", ambao wana haja kubwa ya kumsikia Rais anavyoweza kuwasaidia katika kuongoza vita dhidi ya "saratani" nyingi zinazoikumba nchi yetu:umaskini, ubaguzi katika elimu, na kadhalika!

  Mikutano ya hadhara ndio ya wengi!
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Sep 26, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280
  Bongo tambarareeeeeeeeeeeee

  Kuwapata watanzania ni technique ndogo tu, just do something new, hata kaa umewaibia wanasahau, wanakubeba kukusifu.

  Lazima kuna mkono wa mtu nchi hii si bure!!!

  Just imagine mijitu inavyovutika kirahisi, eti atume meseji akijibiwa basi rais mzuri!!!!!

  poleni wanaharakati, mzigo huu ,tunao huuu, wetu huu!!!
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Uzuri wa wa TZ hatujui kushukuru
   
 5. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Bhagosha,

  Hayo mambo ya talk face to face with citizens wanayaweza wakian Hugo Chaves jamani.
   
Loading...