Hongera mkombozi transport Mwanza

Hongera mkombozi transport Mwanza

Masanja Maguzu

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
547
Reaction score
396
Juzi nilikuwa Mwanza wakati nasubiri usafiri wa daladala ilikuja bus mpya kabisa aina ya tata abiria tulipanda kwa nafasi na wote kupatiwa seat za kukaa.

Dereva ana nidhamu, konda nae ananidhamu kabla ya gari kuondoka aliwakumbusha abiria kufunga mikanda ya usalama na kila abiria alipewa ticket yake.

Sikuona mpiga debe akisogea nikauliza niliambiwa kondakta haruhusiwi kumpa hela mpiga debe kwani kila nauli ina hesabu yake.

Niwakati sasa mijini kutumia magari mapya na ya kusasa. Tuachane na hizi gari mitumba kama hiace na coaster. Uwekwe utaratibu wa kutangaza tenda na msafirishaji mwenye magari bora na huduma nzuri kama mkombozi ndio apewe kandarasi ya kusafirusha abiria mijini
 
Mwanza wapo vizuri katika masuala ya entertainment hata kwenye hotel ukarimu na nidhamu ya wahudumu upo juu tofauti na majiji mengine, hivi is it because mameneja wengi wa hotel wanatoka nchi jirani!!?

Nilijifunza jambo pia kwenye usafiri route ya Mwz - Tarime mabasi kadhaa hayazidishi abiria hata mmoja, abiria atapakiwa njiani kama tu kuna mwingine ameteremka, vinginevyo bus ni nonstop.
 
Dereva ana nidhamu, konda nae ananidhamu kabla ya gari kuondoka aliwakumbusha abiria kufunga mikanda ya usalama na kila abiria alipewa ticket yake.

Mwanza wapo vizuri katika masuala ya entertainment hata kwenye hotel ukarimu na nidhamu ya wahudumu upo juu tofauti na majiji mengine, hivi is it because mameneja wengi wa hotel wanatoka nchi jirani!!?

Nilijifunza jambo pia kwenye usafiri route ya Mwz - Tarime mabasi kadhaa hayazidishi abiria hata mmoja, abiria atapakiwa njiani kama tu kuna mwingine ameteremka, vinginevyo bus ni nonstop
 
Umetumwa?Inatofauti gani na daladala nyingine?Kwani imekuwa mwendi kasi?
 
Juzi nilikuwa Mwanza wakati nasubiri usafiri wa daladala ilikuja bus mpya kabisa aina ya tata abiria tulipanda kwa nafasi na wote kupatiwa seat za kukaa.

Dereva ana nidhamu, konda nae ananidhamu kabla ya gari kuondoka aliwakumbusha abiria kufunga mikanda ya usalama na kila abiria alipewa ticket yake.

Sikuona mpiga debe akisogea nikauliza niliambiwa kondakta haruhusiwi kumpa hela mpiga debe kwani kila nauli ina hesabu yake.

Niwakati sasa mijini kutumia magari mapya na ya kusasa. Tuachane na hizi gari mitumba kama hiace na coaster. Uwekwe utaratibu wa kutangaza tenda na msafirishaji mwenye magari bora na huduma nzuri kama mkombozi ndio apewe kandarasi ya kusafirusha abiria mijini

Hivi Tata ni nzuri kuliko coaster?
Btw Hongereni sana ila mmechelewa sana
 
Nilijifunza jambo pia kwenye usafiri route ya Mwz - Tarime mabasi kadhaa hayazidishi abiria hata mmoja, abiria atapakiwa njiani kama tu kuna mwingine ameteremka, vinginevyo bus ni nonstop

Moja ya route ambayo huwa hawajali abiria ni route ya Mwanza --Tarime.
Kwanza: hawajali abiria wao,unaweza kumuomba kondakta punguza sauti ya redio,na akakujibu hatuwezi kupunguza kwa ajili ya mtu mmoja,na hata mkiwa wengi mtaambiwa kama hamuwezi shukeni.

Pili mpka leo bado zipo bus za 3 × 2,wakati wenzenu route za Dar-Tanga,Dar-Arusha,Dar -Dom wana 2×1..

Kampuni ambayo wapo kind kidogo labda Batco.
Lakin Kisire,Zakaria hovyoo
 
Basi wamechuja karibuni baada ya boss wao kutiwa nguvuni, lakini zamani walikuwa vizuri mno
 
Mkuu mi nazungumzia hapo nyuma kidogo.
Wote walianza kujirekebisha baada ya kuona kila abiria hasa wale wanaojielewa kukataa kupanda bus zao na wakipanda Batco,wakaanza kuchukua makondakta ladiez
 
Kondakta huwa hatoi hela kwa teja kwa kupenda, au Mateja wa Mwanza hawana bisibisi?
 
Mkuu mi nazungumzia hapo nyuma kidogo.
Wote walianza kujirekebisha baada ya kuona kila abiria hasa wale wanaojielewa kukataa kupanda bus zao na wakipanda Batco,wakaanza kuchukua makondakta ladiez
Kwa sasa zakaria wako njema wana bus za spain full kiyoyozi na wahudumu wadada wa kijita yaani huduma ni murua sana
 
Kama wapo hivyo sasahv hongera zao.
Bus za spain ni zipi?
Golden dragon?
Higer?
Hyundai?
Scania?
Volvo?
Tesla?
M,Benz?
Marcopolo?
Tata?
 
Mkuu mi nazungumzia hapo nyuma kidogo.
Wote walianza kujirekebisha baada ya kuona kila abiria hasa wale wanaojielewa kukataa kupanda bus zao na wakipanda Batco,wakaanza kuchukua makondakta ladiez
Kuacha kupanda Zakaria na kupanda BATCO ilikuwa ni issue ya kisiasa. Zakaria ni CCM hivyo wakazi wengi wa Tarime ni wafuasi wa CHADEMA ndio maana walikuwa wanapanda BATCO. Ukimuona mtu amepanda ZAKARIA ujue amekosa nafasi kwenye mabasi ya BATCO
 
Back
Top Bottom