Nadhani bila ushabiki, tunahitaji kuwa na mabadiliko ya sheria ya uchaguzi ili mtu awe mgombea lazima awe mkazi wa eneo husika katika kipindi cha muda flani hata miaka 3 kabla ya uchaguzi na tuweke sifa zinazomfanya mtu atambulike kuwa ni mkazi wa eneo hilo na utaache huu utaratibu wa eti kisa mtu alizaliwa Usongelani, Mabama, Malongwe, Ng,ambo, Usoke, n.k alafu akapotea miaka karibu 30 alafu anakuja kugombea ubunge. Ukiangalia wabunge walio wengi wa tz hutokea Dar kwenda Dom na wala sio kwenye majimbo yao
Mbunge wangu wa SIKONGE..... Hebu weka maksi zako hapa.
![]()
![]()
Brother Juma Kapuya mnamuonaje lakini?
Nikitangaza nia vigezo vyote vitazingatiwa. na usihofu kabisa kamanda.
Eti huyu alikuwa waziri wa ulinzi!! duu !! sijui tulaumu wanaowachagua ama!!?
Ule usemi wa mh.Zitto kuwa yeye ni mbunge wa Kitaifa unaonekana kuwa unaukweli ndani yake. Hii ni kutokana na kutumia nguvu nyingi kuzungumzia na kutetea maslahi ya taifa na si maslahi ya jimbo lake. Mh. Mnyika J.J hutumia nguvu nyingi kutetea maslahi ya jimbo lake sawa na nguvu ileile anayotumia kutetea maslahi ya kitaifa. Jimbo la kigoma kaskazini kuna changamoto nyingi zinazohitaji utatuzi wa haraka. Mazao ya chikichi,kahawa na ndizi hayajapata
ufumbuzi na uratibu mzuri wa masoko hivyo yameshindwa kuwakomboa wana Kigoma kiuchumi. Tatizo sugu la maji linahitaji ufumbuzi pia. Tunakushauri mh. Zitto uige mfano wa mh. Mnyika J.J
Hata mbunge aliyepita nasikia ni wa kutoka Itigi. Huyu Rage wakati akigombea uenyekiti klabu ya Simba alikanusha kuwa anaishi Tabora (katiba ya Simba inamtaka kiongozi awe mkazi wa Mzizima 'Dar'), bahati mbaya wakaazi wa Tabora kama kawaida yao wakaziba masikio na kumchagua ubunge. Ni aibu, wakati wenzetu wanawabunge wa palepale, Tabora wa kuletewa.Nadhani bila ushabiki, tunahitaji kuwa na mabadiliko ya sheria ya uchaguzi ili mtu awe mgombea lazima awe mkazi wa eneo husika katika kipindi cha muda flani hata miaka 3 kabla ya uchaguzi na tuweke sifa zinazomfanya mtu atambulike kuwa ni mkazi wa eneo hilo na utaache huu utaratibu wa eti kisa mtu alizaliwa Usongelani, Mabama, Malongwe, Ng,ambo, Usoke, n.k alafu akapotea miaka karibu 30 alafu anakuja kugombea ubunge. Ukiangalia wabunge walio wengi wa tz hutokea Dar kwenda Dom na wala sio kwenye majimbo yao
Eti huyu alikuwa waziri wa ulinzi!! duu !! sijui tulaumu wanaowachagua ama!!?
Eti huyu alikuwa waziri wa ulinzi!! duu !! sijui tulaumu wanaowachagua ama!!?
Hata mbunge aliyepita nasikia ni wa kutoka Itigi. Huyu Rage wakati akigombea uenyekiti klabu ya Simba alikanusha kuwa anaishi Tabora (katiba ya Simba inamtaka kiongozi awe mkazi wa Mzizima 'Dar'), bahati mbaya wakaazi wa Tabora kama kawaida yao wakaziba masikio na kumchagua ubunge. Ni aibu, wakati wenzetu wanawabunge wa palepale, Tabora wa kuletewa.
Ndivo inavotakiwa iwe, Rage alipaswa agombee jimbo moja hapo Mzizima kwani ndio makazi yake. Hivi sasa yupo wapi? Kwani hata Dodoma hayupo.Kumbe inabidi tujifunze ku-link matukio aisee, tatizo katiba yetu haijawa wazi kuhusu ugombea ubunge kwani inaruhusu mtu kugombea popote pale anapojisikia (kwa sie watz bara) na ndio maana Lyatonga aligombea Temeke na sidhani kama alikuwa mkazi wa Temeke. Kuna haja la kuliangalia hili pia maana agenda ya kuwa mwakilishi maana yake unajua matatizo ya eneo husika hivyo kama wewe ni Mnyamwezi wa Tabora umekaa muda mrefu wa maisha yako Njombe gombea huko na si kurudi Tabora ambako ulikimbia kitambo unless kama una investment zako kule ambazo kwa namna moja ama nyingine zinakufanya uwe unajichanganya na wana Tabora
Mkuu,tatizo ni kukubali kudanganyika na vizawadi. Watu wanaona miaka nenda rudi maendeleo hakuna na kila uchaguzi kinakuja chama kilekile na ahadi tofauti huku wana mafurushi ya zawadi na watu walewale wanadanganyika tena.Kwahiyo mkuu unamaanishi ni wana Tabora wenyewe ndio wanajitakia?
Unfikiri tatizo ni nini mpaka wanatabora wasiamke na kubadilika?
Huo ndio ukweli mtupu mkuu, wakazi wa Tabora mjini nadhani wamekuwa na mbunge mmoja tu alikuwa akikaa nao nae ni mchungaji Misigalo lakini wengine wote wanaagizwa toka Mzizima kuja kupewa ubunge na kurejea huko. Wakijisikia kutembelea Tabora watafika na kwenda katika vijiwe vya KAHAWA na kutoa 'offer' kibao basi miaka inapita.Mkuu,tatizo ni kukubali kudanganyika na vizawadi. Watu wanaona miaka nenda rudi maendeleo hakuna na kila uchaguzi kinakuja chama kilekile na ahadi tofauti huku wana mafurushi ya zawadi na watu walewale wanadanganyika tena.
bila kuukataa uongo wa CCM maendeleo watayasikia kwa wenzao tuu. Umeona Kigoma inavyokuja kasi kwa ajili ya wale vijana Bungeni?