1. Kuna taarifa kuwa Mbunge wa viti maalum Regia Mtema (Chadema) juzi aligoma kutii amri ya OCD ya kuvunja mkutano wa ndani alipokuwa anazunguza na wananchi wa Kilombero kuhusu sakata lao la ushuru mpya wa mazao ulioongezwa toka sh.1,000 hadi sh. 3,000.
2. "Siwezi kuuvunja mkutano huu kwa sababu sijakiuka sheria yoyote na niko hapa kutimiza majukumu yangu kama mbunge. Mimi ni mbunge wa viti maalum, nina haki sawa na mbunge yeyote katika kuwatumikia wananchi wa sehemu yoyote ndani ya nchi hii na isitoshe mimi nimeteuliwa kuwa mbunge kupitia jimbo hili".
3. "Niliomba kibali cha kufanya mkutano wa hadhara mmekataa, sasa 4. huu ni mkutano wa ndani si wa hadhara".
"Naomba muache kuniingilia ninapotekeleza kazi zangu kama mbunge. Niko hapa kuwasilikiliza wawakilishi wa wafanyabiashara na wakulima ili niweze kushughulikia malalamiko yao." alisema Mbunge.
Baada ya kuona hivyo OCD huyo aliwageukia wananchi waliokuwa katika mkutano huo akiwataka waondoke kwa sababu kungeweza kutokea hatari kwao, agizo ambalo hata hivyo halikutekelezwa na badala yake walibaki na kuendelea na mkutano na mbunge huyo.
My take: Kwa hatua hiyo naamini ni mwanzo mzuri ile adabu ya woga inatakiwa isiwepo hata kidogo wao wapo kwa mujibu wa sheria kama ulivyo wewe, polisi wasijione miungu watu. Kumbuka kauli ya Mwenyekiti wenu aliposema nyie (wabunge wa Chadema) mmeingia bungeni kwa kupitia njia za miiba tofauti na wenzenu wa CCM.
Hongera Regia, naomba wabunge wote wa Chadema wawe na ujasiri wa aina hiyo hasa kipindi hiki tunachoelekea cha kudai katiba huru najua wengi watatishwa, mapambano bado kabisa ndiyo yanaanza.
Mzee William, mimi ningesema kinyume chake; yule OCD kama aliona Mbunge anavunja sheria au amekataa kutii amri yake (akiamini ni amri halali) angewatia pingu kuanzia mbunge na wote humo ndani na kuwafikisha mahakamani. Mbunge hana sababu yeye kasema tu kuwa anatekeleza wajibu wake naamini lilikuwa ni jukumu la OCD kuchukua hatua na ningependa achukue hatua mara moja kumfikisha Regia mahakamani kwa kosa ambaloaliamini amelifanya.
Samahani mzee wangu hua nakuheshimu sana kwa hili umepotokaMzee William, mimi ningesema kinyume chake; yule OCD kama aliona Mbunge anavunja sheria au amekataa kutii amri yake (akiamini ni amri halali) angewatia pingu kuanzia mbunge na wote humo ndani na kuwafikisha mahakamani. Mbunge hana sababu yeye kasema tu kuwa anatekeleza wajibu wake naamini lilikuwa ni jukumu la OCD kuchukua hatua na ningependa achukue hatua mara moja kumfikisha Regia mahakamani kwa kosa ambaloaliamini amelifanya.
Tanzania kuna jeshi la polisi au KIGENGE che MAJAMBAZI wenye Vibali?!!!!!Kwa jeshi la polisi kwa ujumla someni alama za nyakati kipindi hiki si cha ubabaishaji ktk kazi au kutafuta sifa itawavunjia heshima ndogo mlio nayo.
Kwa IGP watendaji wako chini ndio wanatoa image ya jeshi kama ndio maelekezo yako nakupa pole sana. Kama ni swala la uweledi nakushauri uweke watendaji wenye uwezo katika ngazo zote. Watanzania wenye uwezo wapo wengi ndani ya jeshi lako. Hivi kuna performance standards kwa jeshi letu? Je ni kumata kuua raia au ni lipi? Kama huna vigezo vya kueleweka nakushauri mjirekebishe.
Samahani mzee wangu hua nakuheshimu sana kwa hili umepotoka
Kwani vikao vya ndani ni sheria gani iliyovyunjwa, kujua matatizo ya watu wako ni kosa
- Now kama hii habari ni ya kweli, basi huyo OCD anatakiwa kufikishwa kwenye mkondo wa Sheria maana sio siri kwamba amekiuka moja ya sheria muhimu sana ya haki za binadam, zinazolindwa na katiba as a Bill Of Rights, again kama hii habari ni ya kweli basi Mbunge asiishie hapo tu bali amfikishe huyu OCD kwenye Sheria zaidi!
William.