Hongera Mh. Regia Mtema kumgomea OCD

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Kuna taarifa kuwa Mbunge wa viti maalum Regia Mtema (Chadema) juzi aligoma kutii amri ya OCD ya kuvunja mkutano wa ndani alipokuwa anazunguza na wananchi wa Kilombero kuhusu sakata lao la ushuru mpya wa mazao ulioongezwa toka sh.1,000 hadi sh. 3,000.

"Siwezi kuuvunja mkutano huu kwa sababu sijakiuka sheria yoyote na niko hapa kutimiza majukumu yangu kama mbunge. Mimi ni mbunge wa viti maalum, nina haki sawa na mbunge yeyote katika kuwatumikia wananchi wa sehemu yoyote ndani ya nchi hii na isitoshe mimi nimeteuliwa kuwa mbunge kupitia jimbo hili".

"Niliomba kibali cha kufanya mkutano wa hadhara mmekataa, sasa huu ni mkutano wa ndani si wa hadhara".

"Naomba muache kuniingilia ninapotekeleza kazi zangu kama mbunge. Niko hapa kuwasilikiliza wawakilishi wa wafanyabiashara na wakulima ili niweze kushughulikia malalamiko yao." alisema Mbunge.

Baada ya kuona hivyo OCD huyo aliwageukia wananchi waliokuwa katika mkutano huo akiwataka waondoke kwa sababu kungeweza kutokea hatari kwao, agizo ambalo hata hivyo halikutekelezwa na badala yake walibaki na kuendelea na mkutano na mbunge huyo.

My take: Kwa hatua hiyo naamini ni mwanzo mzuri ile adabu ya woga inatakiwa isiwepo hata kidogo wao wapo kwa mujibu wa sheria kama ulivyo wewe, polisi wasijione miungu watu. Kumbuka kauli ya Mwenyekiti wenu aliposema nyie (wabunge wa Chadema) mmeingia bungeni kwa kupitia njia za miiba tofauti na wenzenu wa CCM.

Hongera Regia, naomba wabunge wote wa Chadema wawe na ujasiri wa aina hiyo hasa kipindi hiki tunachoelekea cha kudai katiba huru najua wengi watatishwa, mapambano bado kabisa ndiyo yanaanza.
 
yule mtoto wa fudenge alipokuwa na vikao vya rushwa wakati wa kampeni mbona hawaku mzuia
 
Hivi bado kuna hatari ya usalama? au polisi wanatumia kigezo gani kukubali au kukataa? Walitakiwa waweke wazi vigezo wanavyotumia ili kuepuka usumbufu, kwani wanaoomba kibali ni wasomi, wataelewa ni wakati gani wa kuomba kibali
 
1. Kuna taarifa kuwa Mbunge wa viti maalum Regia Mtema (Chadema) juzi aligoma kutii amri ya OCD ya kuvunja mkutano wa ndani alipokuwa anazunguza na wananchi wa Kilombero kuhusu sakata lao la ushuru mpya wa mazao ulioongezwa toka sh.1,000 hadi sh. 3,000.

2. "Siwezi kuuvunja mkutano huu kwa sababu sijakiuka sheria yoyote na niko hapa kutimiza majukumu yangu kama mbunge. Mimi ni mbunge wa viti maalum, nina haki sawa na mbunge yeyote katika kuwatumikia wananchi wa sehemu yoyote ndani ya nchi hii na isitoshe mimi nimeteuliwa kuwa mbunge kupitia jimbo hili".

3. "Niliomba kibali cha kufanya mkutano wa hadhara mmekataa
, sasa 4. huu ni mkutano wa ndani si wa hadhara".

"Naomba muache kuniingilia ninapotekeleza kazi zangu kama mbunge. Niko hapa kuwasilikiliza wawakilishi wa wafanyabiashara na wakulima ili niweze kushughulikia malalamiko yao." alisema Mbunge.

Baada ya kuona hivyo OCD huyo aliwageukia wananchi waliokuwa katika mkutano huo akiwataka waondoke kwa sababu kungeweza kutokea hatari kwao, agizo ambalo hata hivyo halikutekelezwa na badala yake walibaki na kuendelea na mkutano na mbunge huyo.

My take: Kwa hatua hiyo naamini ni mwanzo mzuri ile adabu ya woga inatakiwa isiwepo hata kidogo wao wapo kwa mujibu wa sheria kama ulivyo wewe, polisi wasijione miungu watu. Kumbuka kauli ya Mwenyekiti wenu aliposema nyie (wabunge wa Chadema) mmeingia bungeni kwa kupitia njia za miiba tofauti na wenzenu wa CCM.

Hongera Regia, naomba wabunge wote wa Chadema wawe na ujasiri wa aina hiyo hasa kipindi hiki tunachoelekea cha kudai katiba huru najua wengi watatishwa, mapambano bado kabisa ndiyo yanaanza.

- Now kama hii habari ni ya kweli, basi huyo OCD anatakiwa kufikishwa kwenye mkondo wa Sheria maana sio siri kwamba amekiuka moja ya sheria muhimu sana ya haki za binadam, zinazolindwa na katiba as a Bill Of Rights, again kama hii habari ni ya kweli basi Mbunge asiishie hapo tu bali amfikishe huyu OCD kwenye Sheria zaidi!

William.
 
Mzee William, mimi ningesema kinyume chake; yule OCD kama aliona Mbunge anavunja sheria au amekataa kutii amri yake (akiamini ni amri halali) angewatia pingu kuanzia mbunge na wote humo ndani na kuwafikisha mahakamani. Mbunge hana sababu yeye kasema tu kuwa anatekeleza wajibu wake naamini lilikuwa ni jukumu la OCD kuchukua hatua na ningependa achukue hatua mara moja kumfikisha Regia mahakamani kwa kosa ambaloaliamini amelifanya.
 
Ndugu zetu mlioko madarakini hivi sasa, napata sana wasi wasi kwamba wengi wenu huenda mkaanza kufa siku si zenu KUTOKANA NA UGONJWA WA SHINIKIZO LA DAMU. Kwetu sisi vijana hatuheshimu sura tena bali tunatii sauti ya HAKI PEKE YAKE hata kama ayaeongea mwenyewe hatumuoni macho kwa macho.

Kwetu sisi, enzi za NDIO MZEE bila ya kutathmini kama SIO MZEE isingefaa zaidi haipo tena!! Kwa sasa bado tunabembelezana na wadhalimu, lakini ngojeni tu kidogo tutakujakuelekezana kilicho sahihi zaidi kwetu sisi vijana ....

Hongera Mhe Mtenga!!! Mawazo HURU yadumu milele!!!
 
Mzee William, mimi ningesema kinyume chake; yule OCD kama aliona Mbunge anavunja sheria au amekataa kutii amri yake (akiamini ni amri halali) angewatia pingu kuanzia mbunge na wote humo ndani na kuwafikisha mahakamani. Mbunge hana sababu yeye kasema tu kuwa anatekeleza wajibu wake naamini lilikuwa ni jukumu la OCD kuchukua hatua na ningependa achukue hatua mara moja kumfikisha Regia mahakamani kwa kosa ambaloaliamini amelifanya.

- Unajua Mkuuwangu Mwanakijiji, haya mambo mengine yanatia sana kichefu chefu, hatujui wala kuheshimu sheria OCD na yeye tayari anaamini kwamba ana nguvu za ajabu sana haya yanaitwa mazoea over sheria, OCD amezoea kuwatisha wananchi masikini wa Mungu wasiojua sheria,

- Mimi nimesoma hapo Kidatu, kuna biashara nyingi haramu kuanzia pembe za ndovu mpaka madini, ndio maana OCD anajiona ni mfalme flani hivi Mheshimiwa Regia, tafadhali mfungulie mashitaka huyo OCD au hata lawsuit ili wenzake huko kwingine wajifunze kuheshimu sheria na wananchi.

William.
 
huyo OCD inaonekana ni mamluki au kihiyo wa sheria za kazi zake na za nchi kiujumla.
 
Hii nimeipenda!
Dada Mtema, umeanza vema...congratulations. Hao ndio waajiri wako 2015, so tengeneza CV nzuri ili muda wa ajira ukifika kazi zako zikupigie chapuo.
Again big up and keep it up!
 
Kama alivyosema Malecela, huyu ni mtu 'mdogo' sana, afunguliwe mashtaka na hii itawafanya watu wengi wa aina hiyo 'wanaojiona miungu watu' kufyata mkia na kujua watu wanajua haki zao!kwa huyu inawezekana wala haimuhitaji Lissu!!
 
Kwa vile OCD huyo hana ubavu wa kufanya ambavyo Mzee Mwanakijiji ameshauri basi Chadema kupitia mbunge wake iwafungulie mashataka Jamhuri pamoja na OCD huyo ili Mahakama iamue haki iko wapi! Regia Mtema awe Rosa Parks wao.

Amandla......
 
Mzee William, mimi ningesema kinyume chake; yule OCD kama aliona Mbunge anavunja sheria au amekataa kutii amri yake (akiamini ni amri halali) angewatia pingu kuanzia mbunge na wote humo ndani na kuwafikisha mahakamani. Mbunge hana sababu yeye kasema tu kuwa anatekeleza wajibu wake naamini lilikuwa ni jukumu la OCD kuchukua hatua na ningependa achukue hatua mara moja kumfikisha Regia mahakamani kwa kosa ambaloaliamini amelifanya.
Samahani mzee wangu hua nakuheshimu sana kwa hili umepotoka
Kwani vikao vya ndani ni sheria gani iliyovyunjwa, kujua matatizo ya watu wako ni kosa
 
Kwa jeshi la polisi kwa ujumla someni alama za nyakati kipindi hiki si cha ubabaishaji ktk kazi au kutafuta sifa itawavunjia heshima ndogo mlio nayo.

Kwa IGP watendaji wako chini ndio wanatoa image ya jeshi kama ndio maelekezo yako nakupa pole sana. Kama ni swala la uweledi nakushauri uweke watendaji wenye uwezo katika ngazo zote. Watanzania wenye uwezo wapo wengi ndani ya jeshi lako. Hivi kuna performance standards kwa jeshi letu? Je ni kumata kuua raia au ni lipi? Kama huna vigezo vya kueleweka nakushauri mjirekebishe.
 
Tanzania kuna jeshi la polisi au KIGENGE che MAJAMBAZI wenye Vibali?!!!!!
 
- Now kama hii habari ni ya kweli, basi huyo OCD anatakiwa kufikishwa kwenye mkondo wa Sheria maana sio siri kwamba amekiuka moja ya sheria muhimu sana ya haki za binadam, zinazolindwa na katiba as a Bill Of Rights, again kama hii habari ni ya kweli basi Mbunge asiishie hapo tu bali amfikishe huyu OCD kwenye Sheria zaidi!

William.

si lazima ,kama Ocd halikubali mkutano uendelee basi hajavunja sheria yoyote,kama mbunge ametimiza jukumu lake la kuwasikiliza wananchi naye yu sawa. Sasa mambo ya kupelekana kwa pilato yanatoka wapi? Ebu tafakari kwanza! Alaf bill of Rights?for what and how for this issue? B constructive bwn!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom