Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
Kuna taarifa kuwa Mbunge wa viti maalum Regia Mtema (Chadema) juzi aligoma kutii amri ya OCD ya kuvunja mkutano wa ndani alipokuwa anazunguza na wananchi wa Kilombero kuhusu sakata lao la ushuru mpya wa mazao ulioongezwa toka sh.1,000 hadi sh. 3,000.
"Siwezi kuuvunja mkutano huu kwa sababu sijakiuka sheria yoyote na niko hapa kutimiza majukumu yangu kama mbunge. Mimi ni mbunge wa viti maalum, nina haki sawa na mbunge yeyote katika kuwatumikia wananchi wa sehemu yoyote ndani ya nchi hii na isitoshe mimi nimeteuliwa kuwa mbunge kupitia jimbo hili".
"Niliomba kibali cha kufanya mkutano wa hadhara mmekataa, sasa huu ni mkutano wa ndani si wa hadhara".
"Naomba muache kuniingilia ninapotekeleza kazi zangu kama mbunge. Niko hapa kuwasilikiliza wawakilishi wa wafanyabiashara na wakulima ili niweze kushughulikia malalamiko yao." alisema Mbunge.
Baada ya kuona hivyo OCD huyo aliwageukia wananchi waliokuwa katika mkutano huo akiwataka waondoke kwa sababu kungeweza kutokea hatari kwao, agizo ambalo hata hivyo halikutekelezwa na badala yake walibaki na kuendelea na mkutano na mbunge huyo.
My take: Kwa hatua hiyo naamini ni mwanzo mzuri ile adabu ya woga inatakiwa isiwepo hata kidogo wao wapo kwa mujibu wa sheria kama ulivyo wewe, polisi wasijione miungu watu. Kumbuka kauli ya Mwenyekiti wenu aliposema nyie (wabunge wa Chadema) mmeingia bungeni kwa kupitia njia za miiba tofauti na wenzenu wa CCM.
Hongera Regia, naomba wabunge wote wa Chadema wawe na ujasiri wa aina hiyo hasa kipindi hiki tunachoelekea cha kudai katiba huru najua wengi watatishwa, mapambano bado kabisa ndiyo yanaanza.