Hongera Mbunge na Meya Chadema Mwanza. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Mbunge na Meya Chadema Mwanza.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Indume Yene, May 13, 2011.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mbunge, meya wamvimbishia msuli mganga mkuu

  na Sitta Tumma, Mwanza
  MBUNGE wa Ilelema Highness Kiwia na Meya wa Jiji la Mwanza Josephat Manyerere wamemtunishia msuli Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo ili kuona namna wagonjwa wanavyohudumiwa.
  Ziara hiyo ilihusisha viongozi wengine wa jiji hilo wakiongozwa na mbunge, walifika hospitalini bila taarifa juzi saa 2 usiku kwa lengo la kuona namna wagonjwa wanavyohudumiwa jambo ambalo mganga mkuu aliyejulikana kwa jina la Dk. Onesmo aliwajia juu akigoma kuwapa ushirikiano licha ya kuwafahamu viongozi hao na kuwatuhumu kwamba wamelenga kubomoa badala ya kujenga.
  Awali viongozi hao walifika mapokezi kujitambulisha kisha kuomba maelezo ya jinsi wanavyohudumia wagonjwa, baadaye walikwenda kwa mganga wa zamu, Schola Mulaly, aliyewapa ushirikiano kwa kujibu maswali aliyoulizwa juu ya utoaji wa huduma kwa wagonjwa wanapofikishwa hospitalini hapo.
  Wakati wakiendelea kupata maelezo hayo, walishuhudia mgonjwa, Janefa Masalu (16) aliyefikishwa hospitalini hapo akiwa na taarifa ya polisi (PF3) badala ya kutibiwa alitakiwa kulipa sh 5,000 kwanza ili atibiwe jambo lililowakera viongozi hao huku mganga wa zamu akiwaeleza kwamba baadhi ya wagonjwa hulazimika kununua dawa wenyewe.
  Kabla ya kufika kwa Dk. Onesmo, ujumbe wa viongozi hao ulitembelea wodi mbalimbali ikiwemo ya wazazi na wajawazito ambapo walijionea ‘madudu' baada ya kuwakuta wagonjwa wawili wakiwa kwenye kitanda kimoja na wengine wakilala bila chandarua.
  Hali hiyo iliwalazimu viongozi hao kumtafuta msimamizi wa hospitali hiyo ambaye alikataa katakata kutaja jina lake ili kuwapa ufafanuzi wa baadhi ya mambo hata hivyo msimamizi huyo alianza kuwahoji sababu za ‘kuvamia' hospitali hiyo usiku.
  "Kwa nini mmekuja bila kutoa taarifa? Siku zote tulishazoea mgeni anapotaka kuja lazima atoe taarifa... sasa ninyi kwa nini mje kwa kushtukiza?" alihoji msimamizi wa hospitali hiyo, huku akiwataka waende ofisini kwake kwanza ili awajulishe wakuu wake wa kazi.
  Kutokana na hali hiyo viongozi hao waliongozana hadi ofisini kwa msimamizi huyo ambaye alimpigia simu aliyedai ni mganga mkuu Dk. Onesmo kisha kumweleza ujio wa viongozi hao. Bila kuhoji, mganga mkuu huyo alianza kufoka kwa madai kwamba ziara ya viongozi hao imelenga kubomoa, sio kujenga.
  "Iweje mje hospitalini usiku bila taarifa? Ziara yenu haina nia njema isipokuwa mmekuja kubomoa," alisema Dk. Onesmo akizungumza na mbunge wa Ilemala aliyemweleza kwamba lengo ni kuboresha huduma na kuona jinsi wagonjwa wanavyohudumiwa.
  "…Sisi hatujaja hapa kwa lengo baya, tumekuja kuona mnavyotoa huduma nyakati za usiku... kwa maana hiyo ziara hii imelenga kujenga na kuboresha! Siwezi kukulazimisha uelewe kwamba nia yetu ni kujenga, bali sisi tunaelewa hivyo tofauti na unavyosema.
  "…Kwa nini umekuwa na wasiwasi? Kwani kuna nini kibaya hapa? Sisi tunaelewa utaratibu wote lakini tumeamua kufanya ziara hii ya kushtukiza usiku kwa lengo zuri na si kama unavyodhani wewe," alisisitiza Kiwia kwenye majibizano yaliyozidi dakika 15 na kuahidi kufuatilia ili kubaini chanzo cha hofu iliyoonyeshwa na Dk. Onesmo.
  Kwa upande wake Manyerere alimweleza mganga mkuu kwamba walitaka kuona changamoto zilizopo ili kutafuta namna ya kuzikabili.

  Source: Mtanzania Daima.


  My Take: Huyu Mganga Mkuu anaogopa nini? Kama hospitali ina mapungufu, uongozi unahitaji kuthibitisha hilo kisha kutafuta suluhisho. Haya mambo ya taarifa kabla ya ziara ndo mnapata mwanya hata wa kuchezea vitabu vya mahesabu. Public Domain haijui ni kiasi gani cha fedha kinatengwa kwa ajili ya hospitali hii. Je hizo pesa zinatumika kama ambavyo imekusudiwa?

  Kuna kitu nafikiri huyo Mganga Mkuu anajaribu ku-cover up. Hapa ndipo utapata picha kamili ni kwa nini CCM haitaki kufuata sheria kwenye chaguzi Arusha Mjini. Kuna vitu vinafichwa, kuna connection nyingi sana katika ulaji wa pesa za walala hoi.

  Kudoz Kiwia na Manyerere. Tunahitaji kusafisha hizi taka na kuwatumikia wananchi kama mlivyoapa kwenye viapo vyenu.
   
 2. I

  Igembe Nsabo Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani hujui kwanini anakataa ujio usio na taarifa!! anajua mambo mengi yatajulikana, wakati wao wamezoea kuficha ili waendelee kuonekana ni watenda mema kwa jamii.
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Anataka kujulishwa ili aandae bahasha kubwa na supper ya nguvu kwa mbunge wetu...ndo watendaji wanavyofanya siku hzi,HAAATUDANGANYIKIIIIIIIIIIIII
   
 4. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Watendaji wengine ovyo kweli baada ya kuanisha matatizo anayaficha na kuyatetea,au anajua atakapoeleza matatizo ataiumbua serikali ya magamba na mwisho wa cku ataambulia kuhamishwa?asiwe muoga ktk masuala yanayohusu afya za watu,sera mbovu ndizo zinaperekea huduma mbovu
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni Chama Tawala kimekuwa Madarakani Muda Mrefu; Wizara ya Afya inatakiwa kuwa neutral lakini sababu Waziri ndio kwa Uangalizi wa Ikulu ndiyo inayochagua Waganga Wakuu Nchini anakuwa anitumikia CCM kuliko kuwa mtu asiye na Chama.

  CCM ina Mizizi kila Mahali na Katiba Mpya kama wananchi hatausishwa Rais hatanyimwa Madaraka ya Kuteua Watu

  Only option is we need Change na kuondoa hiyo Mizizi ya CCM hadi kwenye Kata
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  safi sana,..
  walitaka wapewe taarifa ili watandike mashuka mapya?
  au wahamishe wanao lala wawili kitanda kimoja?

  kama wamezoea kuona wakuu wengine wanatoa taarifa hadi
  bara bara zina safishwa hapa wamepatikana kweli
   
 7. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Wanaume KAZINI!!!!
   
 8. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ninakumbuka Waziri Dr. Magufuli aliwahi kufanya ziara kama ya aina hii ya kushutukiza
  usiku kukagua mizani ya kupima magari kati ya Dar na Kibaha, lakini hakuwekewa mikwara
  kama hii aliyoweka huyo mganga mkuu Dr. Onesmo. Na alichobaini Dr. Magufuli ilikuwa
  uozo mtupu.

  Huyu mganga mkuu amejiabisha mwenyewe na taaluma yake, kwani ulikuwa wakati muafaka
  kwake wa kuwaonesha hao ma-boss wa city jinsi hospitali ya Sekou Toure ilivyo na hali
  mbaya, wagonjwa kulala wawili wawili, net hakuna, madawa hakuna, You never know
  labda baadhi ya matatizo yangetatuliwa lakini yeye kwa upumbavu wake eti anaficha
  matatizo. Yaani wasomi wa nchi hii utafikiri sio wasomi, mimi nina wasiwasi kama
  huyo kweli ni MD huenda ni clinical officer (no offense intended) na huo uganga mkuu
  ameupata kupitia mlango wa nyuma wakati qualified MD wakiwepo no wonder hajiamini.
   
 9. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Utendaji wa kiCCM huo.Kuna siku hata wagonjwa wataambiwa watoe taarifa kabla ya kwenda hospitali.
   
 10. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Na bado nasikia watumishi wa halmashauri ya jiji la mwanza wamebanwa vilivyo na zile posho za kijinga kijinga walizokuwa wanajilipa hazipo tena na wengine wanapanga kuuza magari yao kwa kuwa pesa ya mafuta hakuna tena.
   
 11. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hii ndio tofauti kati ya mbunge wa chadema na mbunge wa ccm,
  ukonga mbunge kaingia mti, mwanza mbunge yuko kazini, musoma mbunge yuko kazini kakamata mahindi ya wezi, sugu kazini -mbeya, halima kazini- kawe
  ccm azzan--kapingwa stop baada ya kuwa mkweli nda ya chama cha magamba
  ccm muleba mbunge kapingwa mawe
  mwakyembe--- kafukuzwa jimboni na wananchi
  shy--- ccm mbunge kakimbia jimbo
  ubungo ---myinyika chadema yuko kazini
  kigoma ----zitto kazini
  bunda----- yule tyson watu hawamtaki kawapiga changa la macho la matatizo yao
  tarime---nyambali watu (wana ccm hawamtaki) alitoama matusi kwa mama zao (yakwamba mbunge wa brifcase mama zenu)

  poepleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr


   
 12. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  chadema pigeni kazi ya kutekeleza ilani ya cdm sekta ya afya, ufisadi wa sekou toure unatisha na mbaya zaidi ni wanasiasa wa ccm ndio wanaoikamua hospitali, angalia bodi ya hospitali wajumbe wake akina gachuma (alikuwa mwenyekiti kwasasa sijui) huwa wapo macho sana na mgao, pia ktk hospitali hii wanasiasa wananguvu kuliko RMO na maamuzi yote huwa ni wao wanaamua, msiwalaumu sana madaktari
   
Loading...