Baada ya mashambulizi ya Western Gate, tuliona ukaguzi wa watu na magari ulianzishwa pale Mlimani City shopping mall; ajabu baada ya mwezi wakaacha. Sijui waliwasiliana na Al Shabab wakawaeleza tumeahirisha kuja!!! Hivyo basi, ninahofu hata hilo zoezi la hapo kivukoni si endelevu, Tanzania tunapenda sana kufanya mambo kwa matukio kukiandamana na kupiga pesa ndefu, mfuko tu ukikauka na zoezi linakwisha!!!