S.Liondo
JF-Expert Member
- Apr 20, 2011
- 3,408
- 1,712
Mkuu, hapo ndipo tulipoteleza kama Taifa. Huwezi kuwa na lugha mbili za kufundishia. Nimekuelewa mkuu na kama ulinipata ni kwamba tatizo liko kwenye msingi. Msingi wa lugha hujengwa katika elimu ya awali na msingi, sisi tunajenga kiingereza chetu kwenye msingi wa kiswahili ambao tumewekewa kwenye shule zetu za chini. Ukweli hatutaweza kuimudu lugha hii kwa njia hii. Na haifai kwa mtanzania kushindwa kukijua kiingereza ukitilia maanani kwamba Tanzania ni moja ya nchi za kiingereza. Maana mataifa yamegawanyika katika matabaka ya lugha: Nchi za kifarasa, Kiarabu, kireno, n.k.Mkuu bado hujanielewa huyo mkorea hakusomea udaktari wake kwa kiingereza,sisi ni tofauti masomo yote ni kiingereza na bado ufike hadi PhD bado hujakiielewa hapo ndipo penye swali badala ya kusema ni lugha kama lugha nyingine tukosoe mfumo wa kutumia lugha mbili kufundishia kitu kinachowachanganya wanafunzi.