Hongera Lowassa kwa Shule za Kata

Nyota Ndogo

Senior Member
Aug 7, 2011
150
33
hakika katika mafanikio ulowahi kuyapata katika himaya yako ni kujenga shule za kata.

zimesaidia sana katika ku-promote uhuru wa fikra wa vijana/watoto wa Kitanzania. vitoto vidogo vimemaliza shule ya msingi juzijuzi tu lakini vina taarifa ya mambo mengi mema na mabaya yanayoendeshwa na serikali yetu. hii itasaidia sana pale vitakapotimiza umri wa miaka 18 kutoa maamuzi magumu ya kuendesha harakati za kuiangusha ccm kupitia sanduku la kura.

na uzuri wa shule za kata ni kwamba wanafunzi karibu shule nzima wanatokea kata moja. kwa hivyo kama kata husika raia wake wanaishi maisha ya mlo mmoja kwa siku basi hasira zao kwa magamba ni mara mbili ya mlo mmoja.

CCM sijui watafanya nini sasa? watazifunga shule hizi au vipi? maana kadiri siku zinavyozidi hali inazidi kuwa tete. Watanzania wazee kwa vijana wanazidi kufunguka kifikira.

hongera bwana Ngoyai.
 
Jiulize muda wote huu hujapata hata mtu wa kuijadili thread yako uchwara hajapatikana. Kamuimbie taarabu kitandani kwake huyo unayempamba.
 
avatar yako tuu inatishia kuchangia sijui wewe ni al shabibu
 
Jiulize muda wote huu hujapata hata mtu wa kuijadili thread yako uchwara hajapatikana. Kamuimbie taarabu kitandani kwake huyo unayempamba.

tatizo huyu jamaa hajui kwamba lowassa hasafishiki hata kwa jiki mkuu
 
Mh.lowasa ni mtu mtendaji aliyejichukulia sifa nyingi kwa umahiri wake wa maneno machache yanayotekelezeka.

Akiwa Waziri Mkuu aliweza kuanzisha ujenzi wa shule za kata akiwa na lengo zuri la kumuondoa yule adui ujinga, kumuondoa adui ujinga kungeleta muendelezo wa kumfukuza maradhi na Umasikini.

Kwa ss Mh. Anazungumzia elimu,elimu, elimu hii ana maana Mh. Ana mwarobaini wa tatizo kwa kuwa hakupata muda wa kumalizia kazi hii aliyokua ameianza. Tukimpa nafasi atabadilisha hali ya shule hizi na kuzifanya ziwe kimbilio letu na vizazi vijavyo.Tulianza pamoja, tukahuzunika pamoja na tutashinda pamoja.

Nawasilisha
 
Acha mambo yako ya ajabu Lowasa fisadi ataweza wapi kuendeleza maskini wakati kawaibia mpaka basi aende zake huko mpeleke kwako awe kiongozi wako na familia yako.
 
Watu malofa kabisa.

Spid ya lowasa ile ilikuwa kampeni zake akiwa madarakani ili kujipalilia 2015, lowasa si mtu safi ni uzao Wa panya ni walewale magamba na. Majambazi

Huwezi mtofautisha lowasa na kikwete ni kitu kimoja, tutegemee madudu zaid ya haya ya kikwete kama tutampa nchi lowasa

Huo utendaji wanaosema lowasa anao ni upi? Kwani kikwete hakuwa nao? Waliingia madarakani wote wakiwa na spid na mwisho ziliishia ukingoni na. Wengine uwaziri mkuu hata mwaka hawakumaliza.

Kikwete alianza na mbwembwe mara ghafla kavamia kariakoo, katoa pesa mfukoni nakuwapa watu, leo yupo wapi ndie rais mbovu kabisa afrika hata wa somalia ni imara, rais dhaifu, anaefuraia kushinda kwenye mahoteli marekani, wakati nchi yake haiwezi hata kuzalisha spoke za baiskel.

Utamtifautishaje sasa kikwete na lowasa wakati hawa ni boys two men? Hawakukutana sokoni, nazani tofaut yao kubwa tu ni Kuwa lowasa amekaa mda mfup madarakani kama waziri mkuu kikwete kakaa miaka 10

Otherwise tukifanya makosa kumpa Lowasa nyumba hii, Tanzania, nikumpa fisi mbuzi awapeleke machungani
 
Back
Top Bottom