Hongera Kwenu BBC na Dw Radio

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Kwa miaka mingi kwa hapa east afrika mmekua mkituletea habari motomoto katika nyanja zote,Siasa,uchumi,biashara, michezo na habari zinazojiri duniani

Muendelee na uwajibikaji huo pia kuzipa challenge radio zetu zilizojaa kama utitiri kwa sasa lakini maudhui yao ni kuigana vipindi na kutofuatilia habari kwa kina Bbc/Dw wamekua wakitangaza habari na matukio hata ya ndani kwa uwazi na upana kulikoni vyombo vyetu!

Kibaya ni ile Bbc radio iliyokua inapatikana kwenye frequency za 103.6 miaka michache iliyopita imeondolewa kabisa!

Ile ilisaidia sana kutupa habari na matukio kwa kadri yalivyokua yakitokea duniani kwa 24hrs...

Siku hizi redio zetu mchana ni bongo flava na singeli tu...usiku ni elimu ya mapenzi na dini. ! Hakuna redio inayojielekeza kwenye current news mfano sasa hivi kuna corona lkn fungulia sasa hivi radio zetu usikie kama wanagusia lolote kuhusu balaa hilo la dunia!

Hongereni Dw,Bbc tunasubiri saa 12.30 kupata updates za yaliyojiri duniani leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna haja ya radio zibadirike,ila hizo radio zina Sera zake kamwe haziwezi fanana na radio za hapa nyumbani.
 
Tembo kumlinganisha na sungura siyo jambo la kusameheka, kamwe.
 
Changamoto na hoja zipo nyingi tu za kutangaza mfano kwa sasa maswala ya ajira,shida kwenye kilimo nini kifanyike nchi isonge mbele na matatizo yapungue kwenye afya na elimu lakini wapi redio zetu wame stuck kwenye
Kuchambua mpira,mapenzi ibada na mahubiri ya kutajirika 24 hrs
Bongo flava,Singeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom