Hongera kwa Waziri Mchengerwa kwa kuja na hii sera ya uwekezaji katika uzalishaji wa dawa na vifaa tiba

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
38,534
Reaction score
31,198
Kinachosumbua mawaziri wengi kwa sasa ni namna gani wanafanya shughuli zao kwa mujibu wa matakwa ya mgawanyo wa madaraka na utendaji kazi.
Wengi wa mawaziri wanaacha kujikita katika kubuni na kushawishi mabadiliko ya Sera na muelekeo wake na badala yake wanajigeuza kuwa watu wa kurepond kwenye matukio .

Kazi muhimu ya Waziri ni kuja na sera au maono mapya ili kutatua changamoto za muda mrefu zinazojitokeza kwenye jamii au zitokanazo na utekelezaji wa sera au miongozo iliyopitwa na wakati.

Kazi hii niliyoitaja hapo juu haifanywi kwa weledi na hivyo kupelekea drama au kitatua vijimambo vidogo vidogo huku mizizi ya changamoto ikiendelea kukuwa.

Tanzania imekuwa na changamoto kubwa za msingi zinazohusu afya hususani upatikanaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na utegemezi wa wahisani katika afya.

Ni jukumu nyeti kwa Wizara,waziri na tumu yake kutatua changamoto hiyo iliyianza toka tunapata uhuru.

Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya katika kipindi cha miaka takribani 15.
Leo hii vituo vya huduma pamoja na vifaa vya kisasa vinapatikana katika uwigo wa kilometa 5.

Kinachobakia kama changamoto ni uwepo wa mkakati au sera au maono YA viongozi wa Wizara au sekta ya afya pamoja na watendaji wake ili kuifikisha afya ya jamii kwa wote mahala pazuri na uendelevu wake.

Mojawapo ya maamuzi ninayoayaona yanafanyika sasa kuhusiana na sekta hii muhimu ni pamoja na kuanza utekekezaji wa bima ya Afya kwa wote.
lakini pia kimya kimya ni uanzishaji wa uwekezaji katika viwanda ndani ya nchi venye kutoa huduma katika sekta ya afya.

Tahadhari muhimu inaypaswa kuchukuliwa sasa ni kuwa isijekuwa Wizara ya Afya ikageuzwa kuwa dalali wa wafanyabiashara wa Afya ,badala yake iendelee kwa umakini na uangalifu mkubwa kuhakikisha kuwa uwekezaji katika sekta ya afya unafuata misingi ya katiba yetu yaani UJAMAA NA KUJITEGEMEA.

Hapa nisisitize kuwa pamoja na mabadiliko makubwa duniani kuhusu sera za kiuchumi na uhuru wa soko kamwe tusithubutu kusahau kuwa bado wengi wa watanzania ni masikini wa kutupwa na bado wanahitaji huruma,upendo na muelekeo wa kuwaokoa dhidi ya maradhi na pia gharama za tiba.

Nisisitize zaidi kuwa Tanzania isijiingize kwenye Sera chafu kama walizonazo mataifa "tajiri" ambao yanalalamikiwa na wananchi wao kukosa "access" ya huduma bora kutokana na kipato.

Tusiige mifano mibaya ya marekani au uingereza au mataifa beberu yanayofanya sekta ya afya kama ni biashara na uchumi bali tujikite na kukumbuka kuwa sekta ya afya ni huduma.

Ushauri ambao Mhe.Waziri Mchengerwa hawezi kuupata kupitia wizara yake ya sasa ni pamoja na kutambua asilimia zaidi ya 80 ya watanzania wahitaji,wapiga kura kindakindaki wa CCM ambao wapo chini ya Wizara ya OWM TAMISEMI kwa sasa ndio wanufaika namba moja watakaoguswa na sera mpya za Afya.
Ni muhimu sana mabadiliko yote ya kisera yahusuyo Afya yakawahusisha watumiaji au wanufaika halisi na sio kundi la wachache.
Hapa nasisitiza juu ya kupata maoni halisi kutoka kwa wananchi na kuyachambua maoni kupitia approach ya bottom up na sio top bottom.

Aidha kama waziri wa kisekta ni muhimu kuichungulia sekta kutokea ngazi ya chini yenye kuhusisha jamii na wataalamu wanaofanya kazi ngazi hiyo ya chini.
Bila kufanya hivyo utajikuta umewekeza kwenye mambo makubwa ya kimataifa huku mambo ya msingi yanayowagusa wananzengo yakibaki kama malalamiko na hivyo kuongeza chuki ya wananchi dhidi ya serikali.

KWA HISANI YA MTU WATANZANIA!!
 
Tayari mmeanza kusuka mipango ya kujichotea mahela. Pigeni, utawala wenu huu. Ila mkumbuke malipo ni hapa hapa duniani
 
Mradi wa upigaji huu, hadi kufika 2030 Hazina iko tupu.
Lol
 
Kuhusu matibabu Uingereza? Are you informed? Au unaandika unavyowaza
 
Wewe Unajua sera ya afya ya Uingereza? Usiandike vitu ambavyo huvijui.

Uingereza afya ni bure kwa mtu yeyote anayeishi Uingereza kihalali. Uingereza hawana bima ya afya. Afya hugharamiwa kupitia kodi na hivyo kama huna kipato bado unapata huduma ile ile ya afya sawa na anayopata milionea au waziri.

Wao wanaita wana free at the point of use.

The NHS provides a comprehensive service, available to all, free at the point of use.”

What “free at the point of use” means
  • You do not pay to see a doctor or nurse
  • You do not pay for emergency care
  • You do not pay for hospital treatment
  • Care is based on clinical need, not ability to pay
Muwe mnatumia mifano ambayo mna uhakika nayo.
 
nipo well informed
Haupo informed kabisa. Bora ukubali ukweli kwamba huna ufahamu wa mifumo ya nchi zingine kama vile Uingereza.

Uingereza afya ni bure asilimia 100 kwa mwananchi yeyote. Uwe tajir au maskini, huduma za afya ndani ya shirika la afya la Uingereza (NHS) ni bure.
 
Kulipa wazabuni tu pasua kichwa, hizo ni sarakasi za kawaida kwa hao akili ndogo.
 
Back
Top Bottom