Hongera kwa Polisi, Mtandao wa Majambazi wakamatwa Dar

Nicodemas Tambo Mwikozi

JF-Expert Member
Aug 13, 2016
663
1,047
Mchanganuo wa vihusika vilivyokamatwa
Smg 3.
Pistol 16
Pump Action 3
Risasi s/gun 130
Risasi smg 260
Risasi pistol 526
Radio call 12
Pingu za plastic 3
Pingu za chuma 45
Mkasi 1
Panga 1
cctv camera 1
Gari aina ya Noah 1
Michimbiko ya kungolea mageti 3
Sare ya polisi pea 1. mpaka sasa watuhumiwa watatu mwanamke 1,na wanaume 2 ,

Wale majambazi waliokuwa wamepora maeneo ya veta jengo la sofia house wakiwa wamevalia sare za polisi na kupora pesa wakiwa na Noah yamekamatwa maeneo ya mbagala na mwanamke mmoja kakamatiwa maeneo ya bunju huko ndiko viliko kutwa vitu vyote vilivyo porwa taarifa kamili baadae
Nb na sare nazo zimepatikana
*C&P*
1472936568283.jpg


1472936591562.jpg


1472936607463.jpg


========

UPDATE: 05/09/2016

POLISI KANDA MAALUM DAR WAVUNJA MTANDAO WA MAJAMBAZI.

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefakiwa kukamata watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi hatari ambao wamekuwa wakishiriki matukio mbalimbali ya uhalifu kwa kutumia silaha.

Watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi walipatikana na bunduki 23 za aina tofauti tofauti, Risasi 835, kifaa cha kuzuia risasi kuingia mwilini tatu (Burret Proof), Sare za Polisi, Pingu 48 pamoja na Radio 12 za mawasiliano.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya kanda maalum, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amesema kuwa majambazi hao walikuwa na mtandao mkubwa ikiwa ni kununua silaha nje ya nchi kwa ajili ya kufanyia uhalifu katika maeneo mbalimbali.

Kamanda Sirro amesema baada ya tukio hilo timu ya polisi ya upelelezi iliweka mtego na kufanikiwa kukamata majambazi watatu maeneo ya Mbagala, Keko na Kawe.

Kamanda Sirro amesema katika mahojiano walikiri kufanya tukio katika benki ya Habib African maeneo ya Kariakoo 2014 na Stanbic 2014.

Amesema kuwa majambazi walikiri kuwa na wenzao wako katika msitu wa Vikindu.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha kifaa cha kuangalia wakati wakifanya uhalifu majambazi kwa waandishishi wa habari ikiwa ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikitumika na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha bunduki kwa waandishi wa habari ikiwa ni sehemu yabunduki zilivyokuwa zikitumika na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya operesheni walioifanya na kukamata majambazi watatu katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.







 
Safi serikali iwaongezee police vifaa na technology ya kisasa kuwabaini maramoja majambazi.. Mf hii ya TA tukiwa na vifaa maalumu kwa kufunga mkanda tusomeshe wataalaam na kuwa technology mpya hao majambazi uchwara wasingefika hata kwenye eneo la tukio wangebainika mapema.

Imefika wakati serikali ichukue mawazo toka kwa wananchi kuwa nini kifanyike sio top level ndio wanajipanga kutatua tatizo kumbe kwenye lower level wangepata suluhu mapema..

Viva PT.
 
Back
Top Bottom