Kikwajuni One
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 13,142
- 6,947
Nilikuwa Tanga hivi karibuni,likapita gari la matangazo,kukataza wafanyabiashara kupanga vitu nje,pamoja na wanaofanyabiashara barabarani.Inakuwa vigumu sana kwa watembea wa miguu,kupata sehemu ya kupita inabidi upite barabarani,ambapo ni hatari kwa usalama.
Kwa mfano maeneo ya soko la Ngamiani mpaka kuelekea stand ya mabasi ya mikoani,kuna daladala zinapaki maeneo yale,na kuna wafanyabiashara njiani na kwenye baraza za nyumba,inabidi mtembea kwa miguu apite barabarani.
Na kuna wanaoweka vijiwe vya kahawa katika maeneo ya barazani,watu wanajaa mpaka barabarani,kiasi kuwa ni tabu kwa mpita njia.
Ningeomba isiishie kuwatangazia waondoke tu,zichukuliwe hatua za kuwaondoa.Na vyombo vingine vya dola vishirikiane kuwaondoa watu hawa.
Hawa wanaofanya bishara njiani wanakosesha mapato kwa serekali na jiji. Nampongeza sana Mkurungezi wa jiji Tanga kwa kutufikiria watembea kwa miguu.