Hongera kwa IGP Sirro na Polisi wote

Nsema

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
272
466
Binafsi sijawahi kulipenda Jeshi la Polisi kutokana na kuendesha Mambo yake kiupendeleo.

Lakini tangu zoezi hili la Uchaguzi lianze Jeshi la Polisi limekuwa tofauti kabisa na chaguzi za nyuma. Jeshi la Polisi nalipongeza kupitia IGP Sirro nawapongeza Kama ifuatavyo.

1. Ujio wa Tundu Lissu.
Tangu Mh. Lissu akiwa Ulaya alipotangaza kurudi, watu wengi tulihofu pengine kungekuwa na watu kupata vilema na vifo kutoka na mamia ya watu waliojitokeza kumlaki. Hofu ilitanda zaidi hasa pale msemaji wa jeshi la Police alipoanza kuvutana na Chadema. Lakini Busara za Sirro aliepusha na shughuli ikaenda salama.

2. Zoezi la kudhaminiwa kwa Mh. Lissu.
Hii nayo tulitegemea ingeleta matatizo kulingana na mikusanyiko. Lakini Jeshi la Police hasa lile la Morogoro. Wametenda kazi zao na kuthamini kuwa hii nchi ni ya mfumo wa vyama vingi.Kwa hapa mnyonge mnyongeni Ila haki yake mpeni.

3. Uchomaji wa Ofisi.
Kitendo Cha kuchomwa kwa Ofisi na wahuni huko Arusha na Mbeya. IGP ameagiza kutafutwa kwa wachomaji na kuchukuliwa Sheria.

4. Kurushiwa mawe msafara wa Tundu Lissu. IGP kawaagiza kakemea Hilo. Kwa jumla umejitahidi Sana.

5. Na kitendo Cha kuonya matendo ya tume yanayopelekea uvunjifu wa amani nyakati za Uchaguzi.


Lakini pamoja na hayo. Pia naendelea kulisistizia Jeshi la Police kwenye yafuatayo.

1. Kutekwa kwa wagombea.
Mambo haya tunategemea yanaweza kutokea na yameanza kutokea. Mfano huko Mbinga Mkoani Mbeya Diwani aliyeshinda Kura za Maoni Ccm alitekwa na wasiojulikana. Hatujui amepatikana au Laa. Vitendo kama hivi vitaweza kutokea kwahiyo bila kujali vyama vya siasa mlifanyie kazi.

2. Utovu wa nidhamu kwa Baadhi ya Polisi wanachama wa CCM.
Naweza nikasema hivo kwani kipindi Cha uchaguzi 2015 huko Mpwapwa Police walikuwa wanampigia Kampeni Mgombea wa Chama Tawala. Na mbaya zaidi walikuwa wanawatisha wapigakura waliopanga mistari kupiga Kura.

3. Ukamatwaji wa hovyo wa wagombea.
Hapa utakuta wagombea wengi wa upinzani kukamatwa na Police hovyo bila Sababu ya Msingi.Mfano kukamatwa Kwa Mh. Sugu kule Mbeya. Ilikuwa ni Chuki za wazi kwa yule police si dhidi ya Sugu Bali dhidi ya Upinzani.

4. Kuhusu wasimamizi wa Chaguzi.
Hakuna mtu katika Tanzania na Dunia hii kuwa wanaosimamia uchaguzi ngazi ya Majimbo ni wateule wa Rais tena siyo wateule tu bali ni makada wa tiifu wa Chama Cha mapinduzi (CCm). Huu unabaki mtihani mkubwa Sana kwa demokrasia ya vyama vingi. Mtihani unakuja kwenye kumtangaza mgombea sahihi aliyeshinda.Hapa Dunia inatuangalia Sana. Hapa ndipo panapoleta hofu juu ya Amani yetu.

Kamanda Sirro Kama ulivyosema na kuiasa tume. Utaheshimika Sana kama utashirikiana na tume kutangazwa kwa Mshindi halali ili kuepuka Vurugu.

Mwisho Nakupongeza kwa dhati yawezekana mmedhamiria kutenda haki kutokana na Nchi yetu kuwa kwenye mfumo wa vyama vingi.

Tunakuomba mtende haki ili baada ya uchaguzi isitokee kama Zanzibar Bali tuwe wamoja Kama sasa.
 
Bado sina imani kabisa na jeshi la polisi, kiongozi mkuu ni tatizo katika kuheshimu box la kura. Wanachokifanya polisi kwa sasa ni kuhadaa umma kuwa wako fair, lakini hawatatenda haki wakati sahihi.
 
Tunampongeza kwa kauli zake nzuri lakini tunaomba afanye kwa vitendo na si maneno tu ingawa kuna dalili nzuri hasa kwa yale tunayo yaona kwenye mikutano ya mgombea wa upinzani wakati wa kusaka wadhamini.
 
Bado sina imani kabisa na jeshi la polisi, kiongozi mkuu ni tatizo katika kuheshimu box la kura. Wanachokifanya polisi kwa sasa ni kuhadaa umma kuwa wako fair, lakini hawatatenda haki wakati sahihi.
cHADEMA HATA MKIPEWA TUME HURU MTADAI HAIKO HURU, HAMANA CHEMBE YA APPRECIATION MAANA MNAONGOZWA NA SERA YA KUPINGA KILA KITU
 
Mimi namfikilia sana JPM... yeye ni commander in chief of all armed forces -Tanzania . Na alisha sema kwamba kazi ya Uraisi ni ngumu sana na alisukumiziwa tu ... ninachokiona ni kwamba labda atakubali matokeo ya uchaguzi yatangazwe kwa style ya wajumbe wa ccm.

JPM na Lissu wote ni wakatoliki na kanisa kwa sasa lina wakati mgumu kuonesha upendeleo kwa yeyote kati yao... kitachofanyika (speculatively) ni JPM kukubali matokeo kama yalivyo tangazwa bila kuchakachuliwa na kama alivyowatendea wenzake na yeye atendewe vile vile...atayakubali matokea kwa maana ndio njia pekee ya kutubu dhambi ya aliyofanyiwa Lissu.

yeye JPM akiwa kama Raisi , akiwa kama commander in chief na ku-fail kuwapata wasiojulikana .. alitakiwa kubwaga manyanga kwani tukio lile lilifanyika katika macho yake.. kubwaga manyanga ya Uraisi ndio njia pekee ya kutubu dhambi ile ya jaribio la mauwaji ya Lissu... kumbuka hadithi ya Kaein na Abel- Mungi alisema- mbona damu ya ndugu yao inanililia?

Kaini hakuwa na jibu bali kwenda kujificha uvunguni.. JPM mkabidhi Tundu Uraisi kama akishinda kwa moyo mweupe na utubu dhambi kwa niaba ya serikali yako iliyo shindwa kuwapata walio taka kumuua mtanzania Lissu.
 
cHADEMA HATA MKIPEWA TUME HURU MTADAI HAIKO HURU, HAMANA CHEMBE YA APPRECIATION MAANA MNAONGOZWA NA SERA YA KUPINGA KILA KITU

Tuna akili timamu, tunawezaje kupima mwenendo wa utendaji wa taasisi zetu.
 
Pamoja na hayo yote bado kuna vikauli vinavyoashiria kuwa IGP bado ni mwana CCM
Lilikuwa ni swala la muda tu. Mtazame huyu bwege, eti naye ni OCD!


 
Back
Top Bottom