Hongera kaka na mwanajamvi mwenzetu Lemutuz

Feb 27, 2016
109
138
Wana JF,

Ndugu zangu wapendwa wana JF sioni sababu ya kukaa kimya kwa jinsi ambavyo member mwenzetu lemutuz alivyokuwa akiwasaidia jukwaa kuu kwenye kipindi cha malumbano ya hoja kilichorushwa na ITV siku ya alhamis, hoja ilikuwa juu ya madawa ya kulevya. Kama kuna mtu anaweza kuleta humu mchango wa lemutuz mtanielewa nini kilichonifanya niweke bandiko hili.

Hawa watu wanaopewa jukumu la kusimamia, kudhibiti ama kuelimisha jamii suala zima la madawa ya kulevya huwa hawafanyi research ya kutosha, juu ya chanzo cha tatizo, sababu za tatizo, kwanini nchi kwetu hali imekithiri,(reasons) hawana takwimu sahihi juu ya vijana walioathirika, kunaongezeko la waathirika kiasi gani, wanunuzi wakuu, wauzaji wakuu, watumiaji wakuu, waathirika wakuu, nini kifanyike taifa kuepukana na jango hili.

Wanakuja kwenye kipindi na mipango na michakato chungu nzima ili waendelee kula posho za watanzania. hongera lemutuz tunashauri uwe unafuatilia hoja zinazoligusa taifa zikirushwa ITV ili uwe mwiba kwa watu kama wale na pia mtetezi wa wanyonge na victim wa situation kama zile. Wakijua utakuwepo watajipanga waje na takwimu sahihi na ufumbuzi wa matatizo yanayoikumba nchi yetu....."BIG UP BROTHER"

Kikurajembe Original
 
Capturrrrrrrrre.PNG
 
Back
Top Bottom