Hongera Job Ndugai

Hongera Job Ndugai

nuruyamnyonge

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2014
Posts
4,439
Reaction score
2,287
Leo asubuhi katika kipindi cha nipashe radio one nimemsikia naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na mjumbe wa bunge la katiba mh.Job Ndugai akisema, hatuwezi kupata katiba mpya kwa misimamo mikali ya kwa pande zote mbili.

Job amekwenda mbali saidi na kusema wajumbe wengi wa ccm wanamisimamo mikali kila anaye simama anapinga rasimu ya warioba hii haitasaidia badala yake amesema wakae pamoja na Ukawa ili wafanye maridhiano taifa lisonge mbele.

Ameongeza tena kuwa bunge la katiba linawatu wengi sana kitu ambacho kinachangia kila mtu kuomba muongozo na kupoteza muda, amesisitiza lazima ccm wakae chini na kuacha hiyo misimamo yao mikali kwani haitasaidia kupata katiba mpya.amemalizia kwa kushangaa ccm kusema kama takwimu za warioba siyo halali wabunge wa bunge la katiba wanafanya nini kujadili takwimu hewa!

Naomba kama kuna mchambuzi kamsikiliza vizuri nae aje hapa achangie hiyo kauli ya Job. Matusi hayatakiwi humu ndani jikite kwenye mada.karibuni kwa kuchangia.
 
...nami nimeshangaa leo kaibuka na maneno mazuri sijui kazaliwa upya!!! nimependa zaidi pale aliposema kwamba ili tupate Katiba inayostahili kitu MARIDHIANO haikiepukiki, na ili tufikie hayo maridhiano wajumbe hawana budi kuacha misimamo yao pembeni na wote kuwa na kauli moja yenye nia ya kujenga. Hivyo kusikilizana, kukubali kukosolewa ndani ya Bunge ndiyo njia pekee itakayotufikisha pale watanzania wanapopataka.
 
...ni plan b baada ya plan a kushindwa,wanaangalia namna ya kupoza ukawa...
 
Kinachonishangaza na hao CCM ni kwamba wana mashaka na takwimu za Judge Warioba, that is fine. Lakini kwa busara ya kawaida kama wana maahaka na takwimu, wangemuita Judge Warioba kwenye BMK ili kuzitolea ufafanuzi. Na kama angeshindwa kuwaondolea mashaka basi ndio wangekuwa na haki ya kuziponda. Lakini CCM hawataki kufanya hivyo! Guess why? Kuhusu misimamo ya makundi CCM v UKAWA, mimi ningeshauri kama CCM msimamo wao ni serikali 2 na UKAWA msimamo wao ni serikali 3, basi wengekubaliana NEUTRAL MUUNDO yaani SERIKALI 1. Hiyo ndiyo ingekuwa WIN WIN SITUATION for both CCM AND UKAWA
 
Mi nilitarajia baada ya UKAWA kuondoka bungeni ingewachukua CCM less than an hour kupitisha rasimu yao. As long as wana rasimu yao tayari na wanakubaliana kwa 100% kuna haja gani ya kujadili tena...
 
...nami nimeshangaa leo kaibuka na maneno mazuri sijui kazaliwa upya!!! nimependa zaidi pale aliposema kwamba ili tupate Katiba inayostahili kitu MARIDHIANO haikiepukiki, na ili tufikie hayo maridhiano wajumbe hawana budi kuacha misimamo yao pembeni na wote kuwa na kauli moja yenye nia ya kujenga. Hivyo kusikilizana, kukubali kukosolewa ndani ya Bunge ndiyo njia pekee itakayotufikisha pale watanzania wanapopataka.

Hakika atakula pasaka akiwa msafi wa moyo mbele ya mungu na jamii.kwaresma imemsafisha moyo na kutubu sasa yuko safi kufufuka na yesu.hongera job.
 
...nami nimeshangaa leo kaibuka na maneno mazuri sijui kazaliwa upya!!! nimependa zaidi pale aliposema kwamba ili tupate Katiba inayostahili kitu MARIDHIANO haikiepukiki, na ili tufikie hayo maridhiano wajumbe hawana budi kuacha misimamo yao pembeni na wote kuwa na kauli moja yenye nia ya kujenga. Hivyo kusikilizana, kukubali kukosolewa ndani ya Bunge ndiyo njia pekee itakayotufikisha pale watanzania wanapopataka.

Mie namuona ni mnafiki tu anatafuta gia ya kuwarudisha UKAWA bungeni. Nasema hivyo kwa sababu misimamo mikali anayoisema kuwa wajumbe wa CCM wanayo wameipata katika vikao vyao ambavyo nae Ndugai ni mjumbe, kwa nini hajawashauri huko huko? Pili mbona sijamsikia akiongea humo bungeni kuwashauri wenzie kulegeza misimamo yao?
 
Mi nilitarajia baada ya UKAWA kuondoka bungeni ingewachukua CCM less than an hour kupitisha rasimu yao. As long as wana rasimu yao tayari na wanakubaliana kwa 100% kuna haja gani ya kujadili tena...

Ni kweli lakini wale kwa posho huwatoki Dodoma wataendelea mpaka mwisho na katiba haitapatikana.
 
Serekali 3 zinawatesa sana wabunge wengine wanasema hayo ni mawazo ya Waryoba wengine pamoja na Waryoba wanasema kuwa hayo ni maoni ya wananchi.Ndani ya bunge hilohilo wapo wabunge waliolishana yamini kuwa wahakikishe rasimu ya katiba haipenyi ikiwa na maoni ya serekali 3.Wapo wanaopambana kuhakikisha rasimu ya katiba inapenya bungeni ikiwa na maoni ya serekali3 kwa vile wanaamini kuwa hayo ndiyo maoni ya wananchi.Katika hili wabunge walikuwa hawana sababu ya kurushiana maneno machafu kuimbiana tarabu kuongea maneno ya mipashomipasho kama watoto kitu ambacho kimewafanya wabunge wawe kituko mbele ya jamii.Kitu walichopaswa kukifanya kwa vile kuna wanaoamini kuwa serekali 3 ni mawazo ya Waryoba,Waryoba na baadhi ya wabunge wanasema kuwa hayo maoni ya serekali 3 yametoka kwa wananchi kwa vile rasimu inatakiwa irudi kwa wananchi ikapigiwe kura kuliko kuendelea kurumbana wanatakiwa waiache rasimu ya katiba ikiwa na maoni ya serekali3 ili mwananchi ambaye inaonekana kupakaziwa maoni ambayo hakuyatoa akayakatae hayo maoni kwa njia ya kura.
 
Ni mnafiki tu huyu...

CCM wote lao moja, kashindwa nini kuwakanya wenzake kwenye vikao vya ndani ya chama au hata bungeni?

Mbaya zaidi katika tifutifu hili la misimamo mikali aliyewapa kiburi hao CCM ni mwenyekiti wao Ndg Kikwete, kama sio Kikwete leo hii tusingekuwa hapa.
 
CCM walijua kuwa wapo watu wenye akili kama za Ndugai ambao muda wowote wanaweza kubadilika na kufanya kile ambacho wananchi wengi wanakitaka.Ndiyo maana wakalazimisha kura za wazi ili kuwazibiti watu watakao weza kuwasaliti kama Ndugai.
 
Kwani hayo ameyajua leo,mbona hayasemi akiwa mjengoni,au katumwa akasafishe hali ya hewa baada yakuona mambo yamewaelea,

Ni kweli mambo yamewaelemea lakini walau kwa kauli kama hii ya job inaleta matumaini mapya ya kitaifa ili mchakato pengine urudi kwa wananchi wao waseme wanataka muundo upi.
 
Back
Top Bottom