Habari wana JF,
Miezi kadhaa iliyopita uliwekwa uzi na Mahede Mkorofi kuhusu mambo yasiyofaa yaliyokuwa yanaendelea katika shirika la World vision Tanzania.
Pamoja na ukweli kwamba uzi ule haukuwafurahisha baadhi ya viongozi hadi kutumia nguvu nyingi kutaka kujua Mahede Mkorofi ni nani, lakini mpaka sasa ninavyoandika wamelazimika kuchukua hatua zifuatazo:-
1. Wiki moja baada ya post ile kuna wafanyakazi waliongezewa mshahara kwa zaidi ya asilimia 25.
2. Mpaka sasa aliyekuwa Mkurugenzi wa HR ameshajiuzulu baada ya shinikizo kutoka kwenye Bodi ya shirika na wajumbe wengine wa Senior Management Team.
3. Shirika liliwafutia kesi wafanyakazi walioshtakiwa kwa hila za baadhi ya watu na kuomba kumalizana nje ya mahakama bila masharti yoyote.
4. Kiongozi wa Kanda ya babati kuvuliwa madaraka na kuachwa kama manager mradi, kwani ni miongoni mwa watu ambao wamechangia kuvuruga taswira ya Shirika hilo.
5. Hatimaye baada ya kuvuliwa madaraka aliyekuwa kiongozi wa kanda ya Babati, Bi. Pamela Shao, leo amelazimika kuacha kazi maana yapo mambo amelazimika kuyakwepa.
Kwa hayo machache, nina kila sababu ya kutoa pongezi kwa World Vision Tanzania kwa kuendelea kuchukua hatua za kurejesha misingi ya Shirika hilo la kimataifa lenye heshima kubwa kwenye jamii.
Mwisho kabisa natoa pongezi kwa viongozi wa JF kwa kuwa kimbilio la wanaotamani kusema lakini hawana pakusemea, mmelinda haki ya Mahede Mkorofi kama member kwa kukataa kutoa taarifa zake hata mlipofuatwa na National Director.
Amani ya bwana iwe nanyi.