Hongera Jaji Mkuu kutumia uadilifu wa kaisari, kwanini Majaji wastaafu hawatibiwi?, wanasubiriwa wafe tuu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,597
Wanabodi,

Hili ni bandiko kuhusu uadilifu wa Majaji Wetu.

Declaration of Interest
Nimetokea kumfahamu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, wakati nikiwa mwanafunzi wa sheria pale UDSM, Prof. Ibrahim Juma ndio alikuwa Dean. Miongoni mwa matatizo ya wanafunzi wa chuo kikuu, ni tatizo linaloitwa DISCO, ambalo nami kama binadamu mwingine yoyote, tatizo hili lilinikumba, kwa kupata technical DISCO, na hapa ndipo nilipoufahamu uadilifu wa Prof. Ibrahim Juma, hivyo hili ni bandiko la pongezi za dhati kwa uadilifu huu, ambao kwake uadilifu ni asili yake, ambao sasa anautumia katika wadhifa wake wa Jaji Mkuu wa Tanzania, ambapo naamini sasa sio tuu haki itatendeka, bali haki itaonekana kutendeka!.

Uadilifu wa Viwango vya Juu vya Level ya Julius Kaisari.
Kwa mliomsikia Rais Magufuli akimpongeza Jaji Mkuu, kwa uamuzi wake wa kuwafukuza kazi mahakimu wote waliotuhumiwa kwa rushwa na kushitakiwa mahakamani, licha ya wote kushinda kesi, lakini bado Prof. Juma aliamua kuwatimua kazi wote, kwa kutumia kanuni ya uadilifu ya Julius Kaisari, kwamba unapokuwa na ngazi fulani ya madaraka, kama hakimu, hupaswi hata kutuhumiwa tuu!. Kule kutuhumiwa tuu kupokea rushwa, kunakufanya upoteze sifa za uadilifu wa kuendelea kuhudumu kwenye nafasi hiyo. Hivyo ndivyo alivyofanya Kaisari, mke wake alipotuhumiwa tuu, kukosa uaminifu, Kaisari alimtwanga talaka, na akasema kitendo tuu cha mke wa Kaisari kutuhumiwa, kinatosha kumfanya kupoteza uadilifu wa kuwa mke wa Kaisari hata kama hakuna ushahidi. Hiki ndicho Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma alichokifanya kwa mahakimu hao. Walituhumiwa, wakashitakiwa, hawakukutwa na hatia, hivyo walipaswa kurudishwa kazini, lakini Prof. Juma aliwatimua.

Formular Hii ya Udilifu wa Kaisari, Isiishie Mhimili wa Mahakama Pekee, Bali Itumiwe na Bunge na Serikali.
Tukubali tukatae, Tanzania, tunakabiliwa na tatizo kubwa katika maadili na uadilifu kwa baadhi ya viongozi wetu, kuanzia juu kwenye Ikulu yetu hadi chini kwa wananchi.

Ikulu ni Mahali Patakatifu, Mpangaji Anapaswa Kuwa Mtakatifu!.
Baba wa Taifa, alipaita Ikulu ni mahali patakatifu, akimaanisha yoyote ambaye ni mpangaji wa Ikulu yetu, anapaswa kuwa ni Mtu Mtakatifu, na utakatifu huo, uonekane kwa mawazo yake, kauli zake, Maneno yake na matendo yake, ndio maana kulipoibuliwa tuhumu hizi kuhusu Ikulu yetu, sisi wengine wenu tulishauri zichunguzwe, na zikithibitishwa, huyu mtu atakuwa hatufai!.
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na Zile Boeing ni TT, Then Hatufai!.

Uadilifu wa Mashaka wa Bunge, Mahakama na Serikali.
Kuna matukio mengi ambayo yamefanywa na Bunge letu, serikali yetu, na mahakama zetu yanye viashiria wa uadilifu unaotia shaka wa viongozi wetu, au wahusika wakuu. Simaanisha kila ukosefu wa uadilifu au uadilifu unaotia shaka, ni lazima kuna rushwa imetembea, hapana, kuna baadhi ya matukio, ukosefu wa auadilifu ni kwenye thinking tuu erratically.

Mfano, viongozi wetu wote wakuu, wanachaguliwa kwenye uongozi kwa mujibu wa katiba, na wakiisha chaguliwa, wanaapishwa kwa kula kiapo cha utii wa katiba, kwa kuilinda, kuitetea na kuitekeleza katiba, sasa inawezekana vipi akaibuka kiongozi, akazifuta wa haki fulani zilizotolewa na katiba, na akaachwa tuu hivi hivi?.

Kwa mujibu wa kumbukumbu zangu, nilivyofunzwa somo la Katiba na Prof. Shivji, tulifundishwa kuwa Katiba ya nchi ndio sheria mama, sheria nyingine zote zinazotungwa, lazima ziendane na katiba, hivyo sheria nyingine zote zinazotungwa, zinapata uhalali wa kisheria (legitimacy) kutoka kwenye katiba. Sheria yoyote itakayoyotungwa inayokwenda kinyume cha katiba, ni sheria batili, yaani ni void ab initio!.

Ibara ya 21 ya Katiba imetoa haki ya mtu yoyote kushiriki siasa. Bunge letu tukufu, liliwezaje kutunga sheria nyingine zinazokwenda kinyume cha ibara hiyo?. Nikimaanisha hizi ibara ya 39, 67 na 77 za Katiba, na kifungu Namba 39 sheria the Local Authorities (Elections) Act 1979. Ibara hizo na sheria, hiyo, tangu kutungwa kwake, tayari zilikuwa zinakwenda kinyume cha ibara ya 21 ya katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo ni sheria batili!, sasa swali za kujiuliza sheria hizi batili ziliwezaje kutungwa na kupitishwa hadi kuwa sheria bila wanasheria wetu makini kuuona ubatili huu?. Kitu cha ajabu zaidi sio tuu Bunge kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha sheria mama ya katiba, bali bunge hilo hilo lilatunga sheria za marekebisho ya katiba, zikauchukua ubatili huo na kuutumbukiza ndani ya katiba yetu ili kuuhalalisha!. Huku sio kuinajisi katiba yetu?. Haya yote wakati yanafanyika na kutendeka, mhimili wa mahakama wenye jukumu la kusimamia sheria na katiba upo tuu unaangaliwa jinsi katiba yetu inanajisiwa na Bunge!.

Nakuomba Jaji Mkuu, Prof. Ibrahimu Juma, kwanza katika kipindi chako, usiruhusu jamba kama hili linalokwenda kinyume cha katiba lifanyike na mhimili wako upo unaangalia tuu!.

Nakuomba uendelee kuutumia kanuni hii hii ya uadilifu wa Kaisari, kuondoa unajisi wowote uliofanywa kwenye katiba yetu kwa kupata baraka za watangulizi wako, hakikisha mahakama kuu ya kipindi chako, inarudisha na past glory za mhimili huu ikiwemo kuanza kuzitumia the discretionary powers za mahakama yako, kwa kutumia suo moto (act on its own volition), kuilinda katiba yetu hata pale ambapo hakuna mtu yoyote aliyefungua shauri lolote la maombi ya tafsiri za kisheria.

Mhimili wa Mahakama Utafsiri Sheria/Katiba Usisubiri Shauri!.
Kwenye masuala ya katiba, jukumu la mahakama ni kutafsiri sheria. Kunapotokea ukiukwaji wa wazi wa katiba kama kwenye suala la haki za kufanya mikutano za vyama vya siasa, Jaji Mkuu, usisubiri hadi watu wafungue shauri la kutaka tafsiri, vitu vingine viko wazi kabisa, Mahakama nayo ina jicho kubwa, ikiona katiba inakanyagwa, isisubiri hadi watu wafungue shauri la kuomba tafsiri, Mahakama ina jukumu la kulidhibiti Bunge na Serikali kwa ku play its role of check and balance the executive and the legislature.

Licha ya Kulipwa Vizuri na Mafao Bora, Kwa Nini Majaji Wakose Uadilifu na Kujiongezea Chochote Kitu?.
Majaji ni miongoni mwa kada za juu serikalini, wanalipwa vizuri, na wakistaafu pia wana mafao mazuri, kama haya,
View attachment 690243 View attachment 690246

Paoja na malipo mazuri haya na mafao bora, ila amini usiamini, bado kuna double standards kubwa kati ya mafao ya majaji wakistaafu na wastaafu wengine wa ngazi za juu serikalini. Majaji wakiishastaafu, hawatibiwi tena na serikali!. Kumbe thamani ya maisha ya majaji, ni wakati tuu, wakihudumu kama majaji, lakini wakiisha staafu, ukiondoa mafao yao kama watumishi wengine, majaji wastaafu hawatibiwi na serikali, ila wanapofariki, ndipo serikali hujitokeza kuja kuwazika!. Hii Maana yake, Jaji akiisha staafu, afya yake haina thamani tena, ndio maana hawatibiwi, lakini siku wakifa ndipo serikali inajitokeza kugharimia mazishi!. Nilifikiri kutokana na umuhimu wa majaji wetu, uhai wa maisha yao ndicho kitu chenye thamani kubwa kuliko vifo vyao, hivyo majaji wastaafu nao walipaswa kutibiwa na serikali kama viongozi wengine wakuu wanavyotibiwa, na sio wakiugua, wanaachwa bila msaada wowote wa serikali, ila siku wakifa, ndipo serikali inaibuka kuja kuwazika wanapofariki!. This is as if majaji wakiishastaafu, serikali inasubiri tuu watakufa lini ili ikawazike , badala ya kuhudumia kuhakikisha wanakuwa na afya bora ikiwemo kuwatibu!.

Sasa kwenye mazingira kama haya ya watu wanaongaliwa na kuhudumiwa wakiwa kazini lakini wakistaafu serikali inatupa jongoo na mti wake!, katika mazingira kama haya, zikitokea opportunities za majaji wetu kujiongezea chochote kitu katika kipindi chao cha utumishi, utawalaumu?, au majaji wetu watakuwa na uwezo wa kukataa "asante" kubwa kubwa kama zile za Mzee JR?!, au wanaweza kuepuka kujiongezea chochote kitu cha kwenda vakasheni ulaya na kubakisha chochote kitu cha kukufaa uzeeni?!.

Tusiwalaumu majaji wetu kupokea chochote kitu, vinginevyo ukiwa jaji, ukistaafu salama yako ni ukifa mapema, ikitokea ukazeeka na kuishiwa nguvu, utateseka kwa maradhi ya kiutu uzima bila msaada wowote wa serikali, ila siku ukifa, ndipo serikali inaibuka na msaada mazishi kukamilisha safari yako ya mwisho!. Msaada huu wa mazishi una maana gani kwa majaji wetu kama wanaugua na kuteseka bila msaada wowote?. Hata mimi kama ningekuwa Jaji, ninajua nikistaafu ndio mwisho wa kuhudumiwa na serikali kiafya, nitasubiri tuu hadi nistaafu au nitajiwekea akiba ya kustaafu?.

Afya bora na uhakika wa uhai na matatibu kwa majaji wastaafu ni bora kuliko msaada wa mazishi na ile mizinga siku ya mazishi ya majaji.

Hivyo Mheshimiwa Jaji Mkuu, kama majaji wako hawana uhakika wa maajaliwa ya afya za maisha yao baada ya kustaafu, hata kwa kutumia huu uadilifu wa kiwango cha Kaisari, sio tuu utaishia kufukuza kazi mahakimu wote!, bali kuna hatari ya kuwafukuza kazi hata majaji wote, kama mambo yenyewe ndio haya ya accounts za majaji wetu kudukuliwa ili kuona fedha wanazotumia kwenda vakesheni ulaya na hoteli wanazofikia zimetoka wapi!.

Nakutakia kazi njema na hongera tena kwa Uadilifu wa Kaisari.

Paskali
 
Jaji Mkuu yupi?? Huyuu huyuu!!
Sijui.

Nikitazama suala la kesi ya Lema alivyokaa ndani miezi mi 4 kwa kosa linalodhaminika..
Na huyu Jaji Mkuu alikuwepo..!!
Kwanini hakuingilia kati maana Mhimili wa Mahakama ulichafuka sana wakati ule.
Utasema tuna Independent Jaji Mkuu??

Ukilitazama suala la Mbunge wa Mbeya Mjini Mh Sugu anasota rumande kwa kosa lenye kudhaminika..!! Utasema hapa tuna Jaji Mkuu aliye huru kweli.??
Haoni Hakimu wa kesi ya Sugu anavyovuruga Sheria?
Where is he to intervene on this??

Kuna tetesi pia kuwa huyu Jaji Mkuu akiwa pale UDSM alimsaidia Ridhiwan JK kuendelea na masomo alivyokuwa DISCONTINUED ( alivyo DISCO mwaka wa mwisho) na ndio baada ya hapo akapewa zawadi ya Ujaji na JK..
Anyway Mkuu Pascal hili kama unalijua au yeyote atatupa maelezo..

Lakini huyu Jaji Mkuu kwa mtazamo wa jumla hayupo HURU na amekubali mapema kuwa mnyonge wa Executive.
 
Jaji Mkuu yupi?? Huyuu huyuu!!
Sijui.

Nikitazama suala la kesi ya Lema alivyokaa ndani miezi mi 4 kwa kosa linalodhaminika..
Na huyu Jaji Mkuu alikuwepo..!!
Kwanini hakuingilia kati maana Mhimili wa Mahakama ulichafuka sana wakati ule.
Utasema tuna Independent Jaji Mkuu??

Ukilitazama suala la Mbunge wa Mbeya Mjini Mh Sugu anasota rumande kwa kosa lenye kudhaminika..!! Utasema hapa tuna Jaji Mkuu aliye huru kweli.??
Haoni Hakimu wa kesi ya Sugu anavyovuruga Sheria?
Where is he to intervene on this??

Kuna tetesi pia kuwa huyu Jaji Mkuu akiwa pale UDSM alimsaidia Ridhiwan JK kuendelea na masomo alivyokuwa DISCONTINUED ( alivyo DISCO mwaka wa mwisho) na ndio baada ya hapo akapewa zawadi ya Ujaji na JK..
Anyway Mkuu Pascal hili kama unalijua au yeyote atatupa maelezo..

Lakini huyu Jaji Mkuu kwa mtazamo wa jumla hayupo HURU na amekubali mapema kuwa mnyonge wa Executive.

Ni vipengele gani vya kisheria vinatoa dhamana kwa kesi za Lema na hii ya Sugu.

Tusaidie mkuu sie tusofahamu?
 
Mleta mada
mada zako kipindi hiki zimelenga sana kujipendekeza kwa bwana yule...au kuufurahisha upande Wa bwana yule.
 
Mkuu Mayalla, kwanza fafanua kidogo kuhusu "technical DISCO" yako. Kuna wasomaji humu hata hawajui what "DISCO" stands for. Siyo kila mtu kaenda chuo. Pili, bandiko lako linaonekana kushabikia matumizi makubwa serikalini; hasa pale unapopendekeza majaji nao watibiwe nje. Two wrongs don't make it right. Badala ya kushabikia benefits zaidi kwa majaji hebu shabikia hao viongozi wengine wa serikali wenye haki ya kutibiwa nje haki zao zifutwe wote tutibiwe nchini, tunapokuwa tunaishi nchini.
 
Ni vipengele gani vya kisheria vinatoa dhamana kwa kesi za Lema na hii ya Sugu.

Tusaidie mkuu sie tusofahamu?
The purpose of bail , is to shield the individual arrested from being incarcerated prior to his guilt being established in court. soma kifungu cha 65 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, kifungu hicho kinatoa haki ya kupata dhamana. ikumbukwe kuwa sheria mama, yaani katiba ya JMT Ibara ya 15 inatamka wazi kuwa kila mtu ni innocent mpaka pale itakapodhibitishwa kinyume na hivyo na mahakama ya sheria. hata hivyo, police or DPP wanaweza zuia dhamana hata kama kosa lina dhaminika endapo wataamini kuwa kufanya hivyo kutaharibu ushahidi or kwa usalama wa mutuhumiwa mwenyewe. kinachotokea kwa sugu ni matumizi mabaya ya sheria kwa mihimili iliyopewa mamlaka hayo, ili kukomoa upinzani. In summary, makosa yasiyo na dhamana ni:-
  1. Uhaini-treason
  2. Mauaji/murder
  3. Unyanganyi wa kutumia silaha-Army robbery
  4. Makosa yanayohusiana na uhujumu uchumi-economic sabotage
 
Layman like most of many ma CCM mengi ya kupokea kila kitu... down here need to have eaten well and life fulfilled.

Ili usomane nayo.

Alafuu Mkuu Pasco mbona unatumia nguvu nyingi sana. Au kwa vile ni msukuma mwenzio....

Acheni NJAA.
 
Kwa hili la renumeration/stahiki za majaji sikubaliani nalo kabisa. Wanapewa stahiki kubwa na nyingi mno, zingine zinawazidi hata uwezo. Zinaweka mwanya mkubwa sana kati yao na watumishi wengine wa mahakama. Hii ilipelekea kufanyike zengwe katika kumpatia ujaji Ndugu (madam) Malechela -jina hili ni geni miongoni mwa wengi, lakin aliteuliwa kuwa jaji mwanzoni mwa miaka ya 2010 wakati akiwa mahututi hospitalini. hii ilifanywa makusudi ili apate privilege ya kutibiwa na serikali- nje ya nchi. Hata hivyo jitihada za kumtibu hazikufua dafu, bado aliendelea kuwa mgonjwa na hata ofisini hakufika (alijaribu kama miezi miwili akashindwa akarudi nyumbani tu). hapa serikali ilitumia vibaya sana pesa ya walipa kodi, hapakuwa na sababu ya kuteua mtu kama huyu kuwa jaji.

Pia masilahi mazuri ya majaji yalipelekea mwaka 2011 lifanyike zengwe kwenye intake flani ya majaji. Kamati/tume inayohusika na uteuzi wa majaji ilipendekeza majina kumi, lakini yalipofika sehemu flani majina mengine yalienguliwa na kuwekwa majina ambayo hata hayakupendekezwa na tume, cha ajamu mkuu amri jeshi wa wakati huo akapitisha tu, labda aliamini yamepita katika mikono salama. Kwa maneno mengine kuna majaji walipiga misheni town wakapachika majina yao yaende kwenye uteuzi, wakati walienguliwa katika ngazi ya chini kabisa. baadhi yao ni Msajili wa sasa wa vyama vya siasa na mwingine yupo Sumbawanga ndiye mfawidhi kule (huyu ni usalama wa taifa, na hii ndiyo iliyofanikisha kufanya figisu hadi akapata ujaji na hata kupanda vyeo haraka)

Utaamu wa ujaji ulipelekea jaji mkuu mmoja mstaafu (jina kapuni) kumpigania hawala yake hadi akapewa ujaji wakati hajui chochote kabisa katika tasnia ya sheria. Hii imepelekea mama huyo kujistaafisha kwa hiari (sina hakika kama kulikuwa na shinikizo) baada ya kuona awamu mpya inayotaka uchapaji kazi imeingia madarakani, Mama huyu kastaafu pasipo kutoa hukumu yeyote licha ya kuwa jaji kwa miaka kadhaa. Kwa kifupi alikuwa hajui hata namna ya kupata sheria za tanzania au hata namna ya kuendesha kesi.

Sasa huyu jaji mkuu wa sasa, alikuwa mwalimu wangu pale UD. Kipindi flani alikuwa Dean wa Faculty akatukuta tupo computer room (waliosoma kitivo cha sheria kipindi kile wanakifahamu chumba hiki), Heeeeee! Wakati huo sijamfahamu vizuri bwana... Alitukaripia kwa ghadhabu na kusema... Hivi nyie mmekuja hapa chuoni kuchezea komputa au Kusoma?... Watu wazima tukaelewa.. kila mtu akaondoka kivyake kimya kimya, ingawaje hakujua wala kuuliza nini tunafanya mle.

Kipindi cha huyu bwana kama Dean wa faculty alikuwa strict, na ilitusaidia haswa. Kuna kipindi alitakiwa apewe ujaji, yeye na baaadhi ya wahadhiri pale UD, lakini hawakutaka, sikujua sababu kalini baadaye naona waliridhia na wakaanza kupata uteuzi. Mheshimiwa huyu kawa jaji wa mahakama kuu, na punde tu akapandishwa kwenda mahama ya Rufaa. Baadhi ya majaji aliowakuta kwenye kilinge hawakupendezwa na hili, na walinung'unika vya kutosha. Lakini sasa ndio bosi wao... wampende tu.
 
Back
Top Bottom