Hongera Ester Matiko (CHADEMA), Upinzani sio kupinga kila kitu!

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,282
38,359
Sasa nimejua kwa nini ushindi wako ulitangazwa mapema zaidi kati ya majimbo machache waliyoshinda wapinzani.

Umeonyesha utofauti Mkubwa sana kati ya wabunge wengi wa Chadema, wewe ni hazina ya Taifa.
=================
Wapinzani tulikuwa tunapiga kelele sana dhidi ya ubadhirifu uliokuwa unaendelea Serikalini, sasa kinachonifurahisha kwa Rais Magufuli ni jinsi anavyochukua hatua.

Amenifurahisha kusimamisha utumiaji wa fedha za baadhi ya sherehe za kitaifa na kuziweka katika matumizi mengine kwahiyo mimi nampongeza kwa hilo lakini sio kwa kuziondoa sherehe hizo kwani ni kumbukumbu ya nchi yetu’ – Ester Matiko

Nb: Sitashangaa akiitwa msaliti muda sio mrefu.!
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Hongera Mbunge wangu kutambua Pumba na Mchele na kutumika kulishwa maneno na kupigia Debe ila hali wapiga kura Jimboni tuna kero kibao na wewe ndiyo wakutupigia kelele KERO hizo ziishe ima kupungua.Na siyo kushikia BANGO vitu ambavyo Haviwezekani.Mbunge wangu pigia kelele sana Matatizo yetu JImboni.Sura yako tunaifahamu siyo lazima tukuone kwenye LUNINGA utendaji wako JIMBONI/TAIFA ndio PROMO yako.
 
Mmmmmh kwan nani anapinga uzuiaji wa hela hizo tena HASWA ya kukimbiza MWENGE
 
Hongera Mbunge wangu kutambua Pumba na Mchele na kutumika kulishwa maneno na kupigia Debe ila hali wapiga kura Jimboni tuna kero kibao na wewe ndiyo wakutupigia kelele KERO hizo ziishe ima kupungua.Na siyo kushikia BANGO vitu ambavyo Haviwezekani.Mbunge wangu pigia kelele sana Matatizo yetu JImboni.Sura yako tunaifahamu siyo lazima tukuone kwenye LUNINGA utendaji wako JIMBONI/TAIFA ndio PROMO yako.

Sasa hizo kero zitatatuliwa vipi ikiwa huungi mkono kubana matumizi yasiyo ya lazima, au unafikiri kero zenu zitaisha kwa pesa kutoka mfukoni mwa mbunge.!
 
Sasa hizo kero zitatatuliwa vipi ikiwa huungi mkono kubana matumizi yasiyo ya lazima, au unafikiri kero zenu zitaisha kwa pesa kutoka mfukoni mwa mbunge.!
Naona unaitafuta nafasi ya bingwa wa hoja za kijinga. Hebu soma signature ya invisible itakusaidia kidogo
 
Hivi kujenga barabara ya mwenge -Morocco , madawa kupatikana hospital, MSD kufungua maduka yake , watoto kusoma bure, huduma za serikali kuimarika, kushusha kodi ((PAYE) ,kuanza ujenzi Wa kinyerezi two, fly over.Yote haya kwenu chadema ni maigizo??
Haya endeleeni kuzungusha viuno labda mtapata mabadiliko ya ujauzito.
 
Aaah mtafute mtu akutafsiri nilichomaanisha mkuu
Usijali mkuu, kama nimekosea kutafsiri hiyo comment yako niwie radhi....hiyo uliyoandika ni mother tongue yangu.......sorry mkuu....naona hukupenda watu wajue ulichoandika
 
Usijali mkuu, kama nimekosea kutafsiri hiyo comment yako niwie radhi....hiyo uliyoandika ni mother tongue yangu.....na bado nipo hapa Tarime mjini....sorry mkuu....naona hukupenda watu wajue ulichoandika

Usijali mkuu hata mimi nimeamua niandike cha kwetu kidogo
 
Sasa nimejua kwa nini ushindi wako ulitangazwa mapema zaidi kati ya majimbo machache waliyoshinda wapinzani.

Umeonyesha utofauti Mkubwa sana kati ya wabunge wengi wa Chadema, wewe ni hazina ya Taifa.

=================

Nb: Sitashangaa akiitwa msaliti muda sio mrefu.!
Kwani huyi Ester ni CCM? au ni CHADEMA? LAzima ukimpa hongera yy na chama chake umekipa hongera.
 
Hongera Mbunge wangu kutambua Pumba na Mchele na kutumika kulishwa maneno na kupigia Debe ila hali wapiga kura Jimboni tuna kero kibao na wewe ndiyo wakutupigia kelele KERO hizo ziishe ima kupungua.Na siyo kushikia BANGO vitu ambavyo Haviwezekani.Mbunge wangu pigia kelele sana Matatizo yetu JImboni.Sura yako tunaifahamu siyo lazima tukuone kwenye LUNINGA utendaji wako JIMBONI/TAIFA ndio PROMO yako.
Kama haonyeshwi ungejuaje kuwa katoa sifa hizo unazo mpa eti sura unaijua basi usiwe unaangalia TV wote unawajua
 
chakaza kijana wangu....ukweli haupendi kupuuzwa..,bora uwe unakaa kimya,usiwe kama Mmawia.
Wakudadavuwa mie siwezi kuwa kijana wako hata kidogo. I'm retired Govt officer ingawa sikuondoka kwenye utumishi kwa uzee lakini umri wangu mashallah! umeenda na kuwa nje ya ukijana. Usijaji lugha itumikayo, hapa ni jf lazima twende pamoja ili tuelewane.
Mkuu ukweli naupenda sana ila haupaswi kuchanganywa na upotoshaji. Ni sawa uniambie Magu anafanya kazi vizuri sana na mimi nitakubali, kisha ukiona nimekubali unanichomekea "nadhani huyu ni nabii wa Mungu!' Sasa hapo ndio utaniona tofauti kwani ukweli umeupotosha.
JF ni burudani tuu, tusichukiane
 
Back
Top Bottom