Wambugani
JF-Expert Member
- Dec 8, 2007
- 1,757
- 277
Leo magazetini kulikuwa na taarifa kwamba Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe amebaini rushwa katika Mahakama ya Temeke.
Ni hatua nzuri kwa Waziri kubaini uwepo wa uozo wa rushwa katika Mahakama zetu jambo ambalo limekuwa mazoea ya kila mara katika vyombo vinavyopaswa kusimamia haki na utaratibu, jambo lililofanya wananchi kukosa imani kwa Serikali yao.
Tunamsihi asiishie hapo aangalie na Mahakama nyingine, mfano Mahakama ya Mwanzo Karatu, Mkoani Arusha na kuona uozo uliofanywa katika maamuzi , ambayo ni kinyume na sheria. Hii inadhihirisha mazingira ya wazi ya rushwa, ambapo wakaguzi wao wamebaki kuwaangaliza pasipo kuwachukulia hatua.

Last edited: