VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,904
Nachukua nafasi hii adimu na adhimu, tena muhimu, kukipongeza chama changu cha Mapinduzi kwa kuteka songombingo la bomoabomoa. Kama ilivyo kawaida yetu, hatuchelewi kubadilika. Tunabadilika kama kinyonga kufuatana na mazingira. Hatusomeki haraka. Lakini, wao wataisoma namba.
Undumilakuwili wa CCM yetu ni wa kawaida na unatusaidia. Tunaweza saa mbili asubuhi tukasifu, saa nne asubuhi tukaponda. Jioni, tukapenda. Kama chama tawala, mizizi yetu ipo ki-popo popo. Lilipoanza sakata la bomoabomoa, wanachama na wafuasi wa CCM waliunga mkono maamuzi ya Serikali na kuyashangilia. Bomoabomoa ikasifiwa na kushangiliwa.
Wananchi wakawekewa 'X' kwenye nyumba zao. CCM tukashangilia. Wananchi wanabomolewa na kulia hadharani kwa maumivu makali, wanachama wetu wakapongeza na kuwataka wananchi watii sheria. Anajitokeza Mbunge Mtulia wa Kinondoni. Ni kutoka CUF. Akaanza kuwapigania wananchi wake kimahakama. Akafanikiwa kupata zuio la muda.
CCM ikashtuka. Ikagundua kuwa Mtulia angebeba sifa na nyadhifa zote juu ya sakata hili. CCM ikamtanguliza Abdallah Bulembo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu, kupinga zoezi la bomoabomoa. Tupo ambao hatukushangaa. Tukauona mwanzo wa mchezo wa kekundu.
Sasa, CCM na Serikali yake inaona kuwa bomoabomoa haifanywi ipasavyo. Inataka ifanyike kiutaratibu. Waziri Januari Makamba amewatembelea wahanga na kuwaahidi kuwasikiliza na kuwaridhisha. Kigeugeu cha kisiasa ni muhimu. Wananchi wameahidiwa kulipwa au kupewa makazi mbadala. Kukurupuka kwetu hakuonekani tena.
CCM itazoa sifa na nyadhifa. Tumeshinda tena. Hongera CCM yangu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Last edited: