Hongera CCM, tumeshinda tena!

Hongera CCM, tumeshinda tena!

Ndo raha ya kuongoz wajinga,juzi makamba kamiga kijembe mtuli wa CUF leo anaenda eti kuwasalimia wahanag..sanifu tupu
Dawa ya wanafiki kama hawa ni manati tu. Mimi niliitafuta nikaipata.
 
Mkuu hata kama umeziandika zote hizo kwa saa moja tatizo lipo wapi ? Yeye amezuiliwa na nani kutafuta kibarua cha kuanzisha uzi hapa JF?
Kwani kuanzisha uzi nacho ni kibarua? Sikulijua hilo.
 
Hapo kwenye "UJINGA na UPUMBAVU" ungeandika "ULOFA na UPUMBAVU"

Pole hayo ni mawazo yangu ,mawazo yako uandike ulichokiandika.Heshimu mawazo ya wenzako hata kama yanakuudhi
 
Nachukua nafasi hii adimu na adhimu, tena muhimu, kukipongeza chama changu cha Mapinduzi kwa kuteka songombingo la bomoabomoa. Kama ilivyo kawaida yetu, hatuchelewi kubadilika. Tunabadilika kama kinyonga kufuatana na mazingira. Hatusomeki haraka. Lakini, wao wataisoma namba.

Undumilakuwili wa CCM yetu ni wa kawaida na unatusaidia. Tunaweza saa mbili asubuhi tukasifu, saa nne asubuhi tukaponda. Jioni, tukapenda. Kama chama tawala, mizizi yetu ipo ki-popo popo. Lilipoanza sakata la bomoabomoa, wanachama na wafuasi wa CCM waliunga mkono maamuzi ya Serikali na kuyashangilia. Bomoabomoa ikasifiwa na kushangiliwa.

Wananchi wakawekewa 'X' kwenye nyumba zao. CCM tukashangilia. Wananchi wanabomolewa na kulia hadharani kwa maumivu makali, wanachama wetu wakapongeza na kuwataka wananchi watii sheria. Anajitokeza Mbunge Mtulia wa Kinondoni. Ni kutoka CUF. Akaanza kuwapigania wananchi wake kimahakama. Akafanikiwa kupata zuio la muda.

CCM ikashtuka. Ikagundua kuwa Mtulia angebeba sifa na nyadhifa zote juu ya sakata hili. CCM ikamtanguliza Abdallah Bulembo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu, kupinga zoezi la bomoabomoa. Tupo ambao hatukushangaa. Tukauona mwanzo wa mchezo wa kekundu.

Sasa, CCM na Serikali yake inaona kuwa bomoabomoa haifanywi ipasavyo. Inataka ifanyike kiutaratibu. Waziri Januari Makamba amewatembelea wahanga na kuwaahidi kuwasikiliza na kuwaridhisha. Kigeugeu cha kisiasa ni muhimu. Wananchi wameahidiwa kulipwa au kupewa makazi mbadala. Kukurupuka kwetu hakuonekani tena.

CCM itazoa sifa na nyadhifa. Tumeshinda tena. Hongera CCM yangu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Lowassa hajambo?
 
Kuongoza nchi ya "majuha" kama Tanzania ni rahisi sana. Asubuhi baba anatoa amri, mchana mama anaikanusha, jioni mtoto anawapooza na maneno kisha mnashangilia kwa nderemo na vifijo.
 
Nenda pole pole kijana. Kwanza, hizo si nyuzi za siku moja. Pili, uzi wa 3 na 4 sikuanzisha mimi. Acha ushabiki kijana. Jibu au changia hoja.

Mzee Tupatupa

Vijana wamerahisishiwa maisha unaweza kubapa 1.GB kwa 1500 wiki nzima. Tuwaelekeze wale walio wasikikivu na wakaidi huenda wanaelewa zaidi yetu.
 
Ni wa sababu tu nchi hii ina wajinga wengi
Yaani hili tatizo la ujinga ndio silaha kubwa ya watawala na chakutisha zaidi hata hao waonaitwa wasomi hawaoneshi tofauti yoyote na wasiosoma sijui nchi inaelekea wapi!
 
Nilifarijika wanamtandao walipoandika kuwa Samata ni raia wa Congo... hakika hii si sehemu salama ya kuishi kabisa.
 
Maneno yako Tupatupa yanaashiria we ni mwanaCCM yule mtiifu wa kipindi kile cha misingi ya umoja na mshikamano wa kichama hasa katika miiko na menendo sahihi ya chama kuwatumikia wananchi ila acha mafumo we pwayuka tu watakuelewa wanachama wenzako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom