Mtoboasiri
JF-Expert Member
- Aug 6, 2009
- 5,101
- 1,948
Japo Mimi si mkubwa sana kiumri lakini nakumbuka hadi miaka ya 80 hali ya kuomba omba haikuwa kama iliyopo leo hii. Uongozi wa awamu ya kwanza ulihimiza kujitegemea na kupinga ubinafsi.
Baadae neno "wafadhili' likashika kasi. Kujitegemea ikawa ni ujinga. Wasomi wetu nao wakawa hodari wa kujifunza na kufanya "fund raising" hata ikawa ni kozi nzima vyuoni (vinavyotambuliwa na vya uchochoroni).
Ikahamia kwa watu wa kawaida. Unakuta mtu mtu amepinda kidole kimoja basi kimekuwa kilema cha kumfanya omba omba. Unamkuta mtu barabarani na kikopo chake anaimba "mchango wa msikiti, mchango wa msikiti" n.k, n.k. Michango ya harusi kwa kadi nayo ikawa kama ibada (ndoa zimekuwapo tangu enzi na enzi na haikuhitajika michango)!
Sasa hivi kila shillingi mia tunayotumia (posho zikiwemo) zaidi ya 40 inatokana na wafadhili. Yaani tunaomba ili tulipe watu posho (kumbuka kiranja wa nchi keshatwambia kuwa asiposafiri kwenda kuomba tutakufa njaa)!
Sasa tumeletewa sera mpya na magamba: ya kugawa ardhi yetu (wanatuambia wanaikodisha) ili "wawekezaji" walime ili uwezo wao wa kutupa msaada use mkubwa zaidi!
Hongereni magamba, kwa hilo mmefanikiwa.