Hongera CCM kuitekeleza ilani ya UKAWA

Hongera CCM kuitekeleza ilani ya UKAWA

LEVEL

Senior Member
Joined
Jul 4, 2013
Posts
195
Reaction score
51
Tangu mwaka 1961-2015, Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ipo chini ya utawala wa chama cha mapinduzi, mwaka 1992; upinzani uliingia nchini japo miaka ya juzi tu wapinzani wameanza kupata nguvu kisiasa na hivyo kuweza kuumbua mambo mengi ambayo wananchi wengi tulikua hatuyajui wala kuyasikia, hadi leo hii ninapo andika post hii bado tupo chini ya utawala wa chama cha mapinduzi kinachoongozwa na Dr. John Pombe Magufuli.

Nimejaribu kufwatilia utendaji wake alioanza nao pamoja na hotuba yake ya juzi bungeni nikajifunza kitu kimoja kuwa Rais ameshinda kwa tiketi ya CCM ila anafanya kazi kwa kutekeleza ilani ya UKAWA, safi sana UKAWA kwa ilani nzuri ambayo hadi Rais wetu ameona akiifuata mambo yataenda vizuri, safari za nje tuliongea sana, elimu bure tuliongea sana, dawa tuliongea sana, nk

Viva UKAWA hatujashinda urais ila ilani yetu inatekelezwa na CCM.
 
kweli kabisa maguful ni mtanzania nimeamin ilo
 
Ni vema kuwa Mtanzania zaidi, kuliko mwana itikadi zaidi!
Isitoshe hivi vyama sio sera yetu, ni sera ya wazungu ie Neo colonialism, a divide and rule approach
 
ila kama ataazingatia sera za vyama pinzani na kuchukua mambo muhimu yaliyotajwa yatamsaidia katika utendaji wake
 
Hapa mnatafuta sababu ya kujifariji tu; au wenzetu mlikuwa hamfuatilii kampeni ya Magufuli? Halafu dubwasha la UKAWA halikuwa na Ilani ambayo mtu angeweza kuifuata sasa sijui mnazungumzia Ilani gani.
 
Ni vema kuwa Mtanzania zaidi, kuliko mwana itikadi zaidi!
Isitoshe hivi vyama sio sera yetu, ni sera ya wazungu ie Neo colonialism, a divide and rule approach

kwanini hamtaki kukubari kuwa ilani inayotumika ni ya UKAWA/CHADEMA?
 
Wanaosema Magufuli kuchukua Sera ya Ukawa wanaumwa akili zao, kiacheni cha chamapinduzi kina hazina kubwa ya wanachama
 
UKAWA/CHADEMA ndio think tanks wa nji hii kwa sasa wengine wanasubiri kuprajalize kwa wale mlioenda clas, au kokopi na kupesti kwa wale tulionyimwa fursa ya elimu na maCCM
 
Hata kama ni ilani ya yesu, muhimu tunasonga mbele. Tatizo sio ilani bali ni utekelezaji. Nyie cdm mtabaki na maneno tu wakati magufuli anawaboreshea maisha yenu. Sasa ni kazi tu, hatutazami vyama,kabila wala dini.
 
Tuwekee vifungu kutoka ila ya ukawa tuone mimi nina ilani za vyama vyote alivyokuwa anaongea lowasa vingi alichukua toka ilani ya ccm kwenye ilani ya ukawa havipo
 
Watu mnapenda kujifariji. Wakati Magufuli anataja kero na vipaumbele atakavyoanza kushughulikia mlikuwa mnabeza na kujadili nyomi na Deko. Magufuli anatimiza ilani ya CCM. Na ndio sababu alihuburi sana kwamba mabadiriko ya kweli yatapatikana ndani ya CCM.
 
Hivi ukawa ni chama? Kama sio chama basi vipi watakua na ilani?
 
kwanini hamtaki kukubari kuwa ilani inayotumika ni ya UKAWA/CHADEMA?

wapumbavu watabaki kuwa wapumbavu tu....magufuli aliposema atashirikiana na wapinzani napenda kutumia "kambi ya mawazo mbadala",unaweza kuniambia alimaanisha nini?alipokubali kuoipokea ilani ya chama cha ACT unaweza kuniambia alimaanisha nini??
au mlitaka mambo ya maendeleo ambayo yapo kwenye ilani yenu mtekeleze wenyewe?hamjioni kama nyie ni wabinafsi?
kikwete alivokuwa madarakani mawazo yenu yalivokuwa hayatekelezwi mlisema wapinzani wanadharauliwa leo magufuli ameyathimini mawazo yenu bado tena mnalalamika,hamjioni kama nyie ni wapumbavu na malofa?
 
ImageUploadedByJamiiForums1448210420.758654.jpg
 
Haaa??
Kumbe kule kupokea ilani ya ACT ndio kapokea ilani ya Ukawa!!!???
Tangu lini ACT wakawa sehemu ya UKAWA???
 
Back
Top Bottom