Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,862
- 5,680
Wapendwa ni kwamba katika Waraka wa Kitume ulio tolewa na Maaskofu wa KKKT sikukuu ya Pasaka mwaka jana ulikuwa na ujumbe mzito wenye kutafuta kuliponya taifa ambalo kwa maono ya Maaskofu hao waliokuwa wamefunga katika Maombi ya Mwezi mmoja waliona ni vema hatua stahiki zichukuliwe.
Waraka huo ulijulikana kwa jina la "Amani yetu Taifa letu" uligusia mambo mengi muhimu kwa mustakabali wa taifa. Waraka huo ulipangwa kusomwa ktk Makanisa yote ya KKKT Tanzania siku ya Pasaka.
Katika jambo la kufedhehesha kwa Kanisa ni kuwa Waraka huo haukusomwa ktk Dayosisi ya Pwani ambayo Askofu wake ni Malasusa. Habari za uhakika zinaeleza kuwa Kutosomwa kwa Waraka huo kunatokana na Ushawishi uliofanywa na bwana Daud Albert Bashite kwa Askofu huyo na hivyo basi yeye kuamua kusalimisha Mamlaka yake ya Uaskofu kl Kwa Bashite na kumtii.
Bashite hakuishia hapo tu pia aliandika Barua akishirikiana na Magenge yake ya Uharifu kwenda KKKT akiwataka waufute Waraka huo ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa unakemea Matendo ya uvunjaji wa Haki za binadamu hapa nchini. Lakini chakustaajabisha zaidi ni kuwa Bashite alitishia kulifuta kanisa la KKKT eti kwa kuwa linakemea uovu wao wanao utenda.
Lakini Kama Maandiko yasemavyo Mungu hadhihakiwi, Chochote Apandacho Mtu ndicho atakacho vuna. Mungu hashindani na Mwanadamu kamwe. Marekani wamemtaja Bwana Bashite kuwa kinara wa uuaji, utekaji, utesaji na kupoteza watu hapa nchini.
Ni jambo la kujipima kwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani kuwa anachagua upande upi kati ya kushirikiana na Giza au Nuru.
Maendeleo hayana vyama!
Sent using Jamii Forums mobile app