Hongera Air Tanzania, safari mpya zitakuwa na manufaa kwa nchi

Ndugu zangu,

Ni budi kusema "Uwekezaji, Uamuzi Makini wa Rais John Pombe Magufuli katika sekta ya anga sasa waipa nchi heshima. Air Tanzania yatajwa kuwa moja ya mashirika matatu ya ndege yanayotamba Afrika, ikijipanga kwenda Duniani. Air Tanzania joins regional battle for lucrative new routes.

Mungu Ibariki TanzaniaView attachment 1020533
Mmeacha kuwajengea wakulima miundombinu ya umwagiliaji mmeenda nunua midege ambayo itakuja wagharimu watanzania.

Tumeona serikali ilivyogombana na kina zito,Nape na wabunge wa mikoa ya kusini, hata kufikia mkuu wa nchi kutishii kuvunja viuno vya shangazi zao. Hii ilitokana na serikali kupora pesa za wakulima wa zao la kilimo(korosho).

Hili linatuonesha kuwa kilimo kina tija kikiboreshwa na kujengewa miundombinu.
Pia kingetoa ajira ya uhakika kwa vijana wetu hata waliokwenda shule.

NYUKI HUFUATA MAUA,INZI HUFUATA UCHAFU(Mavi)KWAKUWA NDICHO CHAKULA CHAO.
Ni miongo kadhaa sasa tunaona wenye taaluma mbalimbali wanakimbilia kwenye siasa, ni kwasababu kuna uhakika wa maisha bora( KUNALIPA).

Vivyo hivyo kama serikali ingewekeza nguvu kwenye kilimo, ninaamini vijana wengi wanaotoka mashuleni wasingehangaika na bahasha mikononi au kukesha mitandaoni kutafuta kazi,badala yake wangekesha mitandaoni kutafuta masoko na watu wa kufanya nao kilimo ndani na nje. MIDEGE IMEAJIRI WATU WANGAPI?

VIJANA WENGI WAMETOKA VIJIJINI WAMEKIMBIA KILIMO KISICHO NA TIJA.

Ndiyo hao mnaowana wakipiga debe stand,wanauza Mayai ya kuchemsha,Katanga,power bank,memorycards,charger za simu humo stand na sehemu zingine. HAO HAWANA FUTURE.
JE NDEGE ZITAWASAIDIA NI NI KWENYE MAISHA YAO,NA NI LINI?

Wenzetu mnaopongeza kila jambo mnalugha moja mnasemaje, mnafanya hayo kwa ajili ya Vizazi vijavyo,ni sawa.
JE SISI TUNASTAHILI KUISHI MAISHA YA SHIDA KWA AJILI YA HIVYO VIZAZI VIJAVYO?.

Ondokeni kwenye usingizi wa upumbavu enyi kikazi cha laana, maji HUFUATA mkono, ukiishi vibaya mzazi, watoto wako wataishi hivyo hivyo.
Na ukiishi maisha bora yenye maarifa na busara,wanao pia.

Miaka ya 60 watotwachache sana walisomeshwa kwa kuwa wazazi wasomi walikuwa wachache pia. Ndiyo maana msukuma anaona heri Mtoto akachunga Ng'ombe na wakike aolewe,kusoma ni kupoteza muda.
Hii ni kwa Sababu mzazi hajasoma.

UKIISHI VIBAYA USITAZAMIE KIZAZI CHAKO KITAISHI KISTAARABU. WEKEZENI KWENYE SEKTA ZINAZOGUSA MAISHA YA WATU MOJA KWA MOJA.

UNAFUNGA TAI SHINGONI KUTAKA SIFA HUKU CHINI UMEVAA CHUPI BILA SUALI!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom