Hong Nkong wanataka nini, Watanzania wanataka nin?

Hong Nkong wanataka nini, Watanzania wanataka nin?

Nchi za Scandinavian zimeendelea zaidi,sidhani kama utawala wa kiimla umewahi kutumika kwenye nchi hizo
Nakuelewa ila maendeleo ni swala linalotegemea mambo mengi sana miongoni mwayo ni nchi zinazokuzunguka....

Huko nyuma hata hizi nchi za Skandinavia zilikua na falme.

#NaonaLeoUmekunywaDawaSiasaZinapanda😀
 
Mji wa Hong Nkong,nadhani kila mtu ambaye amesoma au anafuatilia dunia anaujua sana,ingawa wengine wanaweza wakawa wamefika au wengine hawajafika ila wanasoma kwenye mitandao na vyombo vya habari

Hong Nkong ni mji uliostawi kiuchumi zaidi,yaani kama ni miundo mbinu ya kila aina ,reli za kisasa,flyovers, barabara,majengo ya kisasa,minara mirefu duniani,utalii,Viwanda vya kila aina nk

Lakini jiulize pamoja na hayo yote,nchi hiyo inakabiliwa na machafuko,waandamanaji wapo barabarani wakitaka Uhuru

Uhuru,Uhuru,Uhuru,uhuru,hawataki wawe chini ya China,bora wawe chini ya Uingereza kuliko kuwa china

Wanajua fika kuwa wakiwa upande wa China ,hawatakuwa huru,watanyanyaswa na China,nchi ya China haitaki Demokrasia

Wahonkong wanataka Demokrasia,wanataka wawe huru,hawataki kuwa na tawala ambazo zinabana Uhuru wao na Demokrasia

Tunaposema Uhuru wa kujieleza ni kitu muhimu kuliko SGR na Bombardier muwe mnaelewa

Hakuna kitu kibaya kwa binadamu kama kumnyima Uhuru au demokrasia, unaweza ukampa kila kitu lakini usipompa uhuru wa kuamua mambo yake,hayo yote ni zero

Wapambe wa jiwe na jiwe wanapokosolewa kuhusu kuwanyima uhuru wananchi,wenyewe huja na majibu mepesi sana,SGR,flyovers,umeme selous,,bombardier, na kumpongeza Jiwe

Viongozi jifunzeni ya Hong Nkong,binadamu anataka nini zaidi?
MKuu unalilia upewe uhuru wa kujieleza wakati uko live unajieleza!
 
Back
Top Bottom