Watu wamechoshwa na Serikali, Dini na Siasa: Wanataka kuwa huru

Watu wamechoshwa na Serikali, Dini na Siasa: Wanataka kuwa huru

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,886
Reaction score
5,172
Katika hali ya kipekee sana Jamii ya Binadamu leo katika maeneo mengi Duniani inaonesha kuchoshwa sana na Serikali , Dini na Siasa. Taasisi hizo ziliiaminisha Jamii kuwa zitaleta utaratibu katikakati ya vurugu " to bring order out of chaos". Watu waliipokea imani hiyo na kukasimisha mamlaka yao kwa vyombo hivi ambavyo kwa sasa haihitaji kufanya utafiti kugundua kuwa vimewachosha wananchi.

Karl Marx alionesha kuchoshwa mapema sana na Dini hadi kufikia kusema Dini ni kilevi cha akili na pumbazo la wengi " religion is an opium of mind". Kauli hii haioneshi kebehi tu ila inaonesha kutokufikia matamanio ya wengi. Watu walichoamini kukipata kwenye Dini walikiona kama " Utopian philosophy". Hali hii ni endelevu mpaka sasa watu wamechoka sana, wanataka kuwa huru.

Licha ya ukweli kuwa Serikali inapata nguvu kutoka kwa watu ambao ni wananchi leo tafsiri hii inakuwa na ukakasi mkubwa sana akilini kutokana na uhalisia ulivyo. Ukweli mchungu ni kuwa Jamii imemuumba Mungu wake na Mungu huyo amekuwa na nguvu kiasi cha kuwataka waliomuumba kuwa dhabihu.

Siasa za Kiimla ziliposhamiri matumaini yaliletwa na Siasa za kidemokrasia. Leo tafsiri tu ya demokrasia kiutendaji ni changamani sana kiasi cha kuwa na demokrasia za kikanda mfano Demokrasia ya Kiafrika (African Democracy). Kwa kifupi njia hii yenye jina demokrasia nayo haihitaji kutumia nguvu kuona uchovu wa wananchi.

Watu wanataka nini basi?. Jibu la haraka sana ni kuwa watu wanataka kuwa huru, Uhuru huo ni upi? Jibu ni kuwa; uhuru wautakao watu ni hakika ya kuishi kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yao tangu mwanzo. Lipo kusudi ndani ya kila mtu na kusudi hilo ndilo linalomsukuma mtu kutaka kuwa huru zaidi.
 
Taasisi hizi zote ukiziangalia zina usuli wa ukasimishwaji wa mamlaka ya watu zikiwaaminisha watu kuwa zitaleta utaratibu na kuondoa vita ya wote dhidi ya wote "war of all against all (chaos)" Matarajio ambayo wengi wanatamani hata sasa.
 
NAchukia dini zinavyo brainwash akili za watoto wadogo wasio na hatia,hasa dini ya kiislam.
 
Mara mia niwe mwanasiasa ntawadanganya mkileta nyenyenye ntaambia wangu "kamata huyo " muingie ndani mlale kuliko dini ambazo zimekuwa kazi yao ni kuvuna kutoka kwa mwananchi usiku na mchana.
 
Mara mia niwe mwanasiasa ntawadanganya mkileta nyenyenye ntaambia wangu "kamata huyo " muingie ndani mlale kuliko dini ambazo zimekuwa kazi yao ni kuvuna kutoka kwa mwananchi usiku na mchana.
Unaona ulivyochoshwa Mkubwa!!!...daaaah watu wamechoka sana
 
Back
Top Bottom