🔋✨ Honda Inachagua Njia Yake! 🚗💨

🔋✨ Honda Inachagua Njia Yake! 🚗💨

black-tz

Senior Member
Joined
Jul 20, 2021
Posts
115
Reaction score
164
🔋✨ Honda Inachagua Njia Yake! 🚗💨

Badala ya kwenda 100% EV kama kampuni nyingine za magari, Honda imesema inawekeza zaidi kwenye magari ya Hybrid na kusitisha mpango wa EV!

Honda na Nissan zilikuwa zimekubaliana kuungana na kuwa kampuni moja lakini mwanzo wa mwaka huu zilisitisha mpango huo; kwa sababu za kutofautiana kimtazamo na Honda ilikataa kuwa chini ya Nissan.

Baada ya muunganiko wake kufeli, Honda imeamua kutangaza kuwa itaweka focus katika magari ya hybrid (HEV) na sio katika magari ya umeme.

Kampuni za magari za Japan na Ujerumani; hivi karibuni zimekuwa zikitangaza kuweka focus kwenye EV lakini soko bado halijaanza kufanya vizuri.

Honda imeona ichukue njia yake kwa kuwekeza kwenye HEV kwa sababu bado zina soko kwa sababu nchi nyingi hasa zinazoendelea bado hazina mfumo mzuri wa kuchaji. Hybrid ni mfumo mzuri ambao unatumia mafuta na umeme. Bado Honda inaona mafuta yataendelea kutumika na kuhitajika hivyo sio vyema kuwekeza katika magari ya umeme peke yake. 💡⛽

Je, ni smart move au watachelewa kwenye future ya EVs? 👀👇

__
 

Attachments

  • IMG-20250606-WA0027.jpg
    IMG-20250606-WA0027.jpg
    57.8 KB · Views: 14
Sio Siri Kati ya watu ambao hatupendi magari ya UMEME Mimi ni namba moja.
Makampuni yote magari nchini Japan wanapendekeza Sana hybrid car kwasababu kama ni kutunza mazingira haya magari ni rafiki. Ndiyo maana hata wajerumani pia bado wanapendekeza hybrid

EVs tuwaachie wachina Kwanza
 
Back
Top Bottom