Homa ya mapafu/Pneumonia au nimonia ni kitu gani?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1610977661334.png

Pneumonia Ni Nini?

Pneumonia ni ugonjwa unaoshambulia vifuko vya hewa kwenye pafu moja au yote mawili. Vifuko hivi huweza kujaa maji au usaha na kusababibisha kikohozi kinachotoa uchafu unaotoka kwenye mapafu, homa na kupata shida katika kupumua. Vijidudu wa aina nyingi wanaweza kuhusika katika ushambuliaji wa mapafu hayo. Mara nyingi pneumonia hutokana na mashambulizi ya bacteria, virusi, fangasi (fungi) au vijiumbe wengine tegemezi (parasites).

Mtu anapovuta hewa yenye wadudu hawa wadogo (germs) wanaosababisha maradhi, wadudu hawa huingia kwenye mapafu na
kama kinga za mwili za mtu huyu zitashindwa kuwazuia, wadudu hawa hukaa kwenye vifuko vidogo (alveoli) vya kwenye mapafu na kuanza kuzaliana. Mwili utakapopeleka chembechembe nyeupe za damu kupambana na wadudu hawa, vifuko hivi hujaa majimaji na usaha na kusababisha pneumonia.

Ni nani anayeathiriwa?​

Watu wa umri wote wanaweza kupata Pneumonia.
 
Siku akifa yule mtoa marufuku ya kutangazwa covid 19 ndipo hiyo nimonia itapotea
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom