Homa ya Lassa yaua watu 41 nchini Nigeria

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Kituo Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza nchini Nigeria (NCDC) kimetangaza habari ya kufariki dunia watu 41 kutokana na kuzuka wimbi jipya la homa ya Lassa nchini humo.

Katika taarifa yake ya jana Jumatano, kituo hicho kimesema kuwa, maambukizi ya homa ya Lassa ambayo huzuka nchini Nigeria kila mwaka katika wakati kama huu, yameongezeka sana katika kipindi cha siku chache zilizopita kiasi kwamba tangu mwanzoni mwa mwezi huu wa Januari 2020 hadi hivi sasa, watu 41 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na homa hiyo.

Takwimu za karibuni kabisa zinazohusiana na kipindi cha tarehe Mosi hadi 26 mwezi huu wa Januari zinaonesha kuwa, watu 258 wamethibitishwa kukumbwa na homa ya Lassa katika majimbo 19 ya Nigeria huku watano kati yao wakiwa ni wafanyakazi wa kupambana na homa hiyo.

Kituo hicho cha NCDC kimeongeza kuwa, mbali na kuthibitishwa kesi 258 hadi hivi sasa, tayari kuna kesi 689 zimeripotiwa lakini hazijathibitishwa zote. Kesi nyingi zimeripotiwa katika maeneo ya kusini mwa Nigeria ya Ebonyi, Edo na Ondo.

Mwaka mmoja uliopita, serikali ya Nigeria ilitangaza kuzuka ugonjwa wa homa ya Lassa nchini humo ambapo katika kipindi cha mwaka uliopita wa 2019 karibu watu 170 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Taasisi ya Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza nchini Nigeria siku chache zilizopita ilitangaza kuwa, imeanzisha vituo vya dharura vya tiba katika kona zote za nchi hiyo baada ya kuenea ugonjwa huo na vile vile kuzuka virusi hatari ya corona huko nchini China.
 
Aisee....mkuu tupe in detail kuhusu iyo homa ya lassa? Ni kitu gani hasa

am better here
 
Back
Top Bottom